Mwanaye na aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin
Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.
Katika ujumbe wa sauti
uliochapishwa katika mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa
Marekani kwa kumuua babake 2011 huko Pakistan.
Ujumbe huo wa dakika
21 wenye kichwa "We Are All Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa
alikuwa na babake makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa ameapa
kuendeleza kazi aliyoianza babake.
'Tutaendelea kuwasaka
na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama
kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia
na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la habari la Reuters
linamnukuu.
'na kwa wale
wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osama ole wenu, kwanini
sisi tutakuwa tukilinda dunia ya kiislamu'' alisema Hamza.
Nyumba Alimouawa OSAMA Mwaka 2011 Huko Pakistan |
Osama aliuawa na
makomando wa marekani katika maficho yake huko Pakistan mwaka wa 2011.
Hamza ambaye kwa sasa
ana umri wa kati ya miaka ishirini hivi alikuwa na babake kabla ya mashambulizi
ya kigaidi ya mwaka wa 9/2001 huko Afghanistan kabla ya kukimbilia Pakistan
kufuatia mashambulizi makali ya Marekani na washirika wake.
Hamza kulingana na
wachanganuzi anatambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman
al-Zawahiri katika ujumbe huo unaolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa
wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.
0 comments:
Post a Comment