Mamia ya watu wamevua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea
utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza.
Tukio hilo ni la
kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
Washiriki walipakwa
rangi ya samawati Jumamosi na kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo
mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa
na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art
Gallery.
Picha zilizopigwa
zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017
itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick, anayetoka New
York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
Amewahi kupiga picha
za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal,
Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany.
Bw Tunick amesema kazi
zake “hugusia historia ndefu ya Sanaa ya utupu”.
"Mavazi ni Sanaa
ya mtu mwingine,” anasema.
“Fashoni ni Sanaa. Kwa
kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika
umaridadi wake.”
Watu karibu 3,000 walihudhuria
kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi Machi.
0 comments:
Post a Comment