Tanzania ina vipaji
vingi na wasanii wengi wa kiume wanaofanya muziki wa Bongo flavour wa miondoko
ya R n B almaarufu muziki wa kuimba.Kati
ya wengi leo tutakuletea wasanii kumi wakali wanaoonekana kuwa na sauti zenye
mvuto na za kuvutia kusikiliza nyimbo zao hasa wanapoimba.
Vigezo vilivyozingatiwa
ni uwezo wao wa kuimba kwa pitch zote za
juu na za chini na kati,uwezo wao wa kuhimili kuimba kwa muda mrefu bila sauti
kuathirika na uwezo wao wa utunzi mwanana.
1.
Ali Kiba
Namba
moja anaishikilia Ali Kiba, mwenyewe hujiita King Kiba.Huyu ni mwanamuziki wa
siku nyingi na tangu aanze muziki wake sauti yake haikuwahi kuchuja.Huyu huweza
kuimba kwa sauti kali sana,kati na hata ya chini bila kukwama wala kukosea.
2.
Barnabas
Anashikilia
namba mbili huyu sio uimbaji tu ni mtunzi mzuri sana wa nyimbo na sio za kwake
peke yake bali hata wasanii kadhaa wamekiri kutungiwa nyimbo na msanii huyu
3.Ben
Pol
Anashikilia
namba tatu huyu ana uwezo mkubwa wa kucheza na sauti yake hata ukaburudika
haswa.
4.Baraka
Da Prince
Huyu
ni msanii mpya lakini alieonyesha kutobahatisha hasa kwa sauti yake ya juu mara
nyingi na tungo murua za mapenzi.
5.Linex
Hujiita
voice of Africa.Huyu sauti yake ni ya kukwaruza ama inayoonekana kutaka kukwama
lakini tungo zake hakika utazifurahia.
6.Christian
Bela
Mwanamuziki
wa muziki wa dansi lakini mwenye kuimba na kutunga nyimbo zisizochuja
kusikiliza.Ana uwezo mkubwa sana wa utunzi.
7.Amini
Amini
yeye ni mwimbaji mzuri na sauti yake ni ya kubembeleza.Ni zao la THT
8.Peter
Msechu
Peter
ni mwalimu wa muziki haswa kwa hiyo haishangazi kumwona kwenye orodha
hii.Anajitosheleza
9.Diamond
Platinums
Huyu
anajulikana haswa kwa kucheza na sauti na midundo.Anavuma kimataifa
10.Mo
Music
Msanii
mpya lakini pindi usikilizapo tungo zake na sauti yake utakubaliana nasi kuwa
anastahili kuingizwa kwenye list hii.
0 comments:
Post a Comment