Kwa mara ya
kwanza shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA imemteua mwanamama Fatma Samba
Diouf Samoura msenegali kuwa katibu mkuu wake.Bi huyu atakuwa mwanamke wa
kwanza kushika wadhifa huo tangu shirikisho hilo kuanzishwa.Bi Fatma anachukua
nafasi ya Jerome Valcke ambae amefungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa miaka
12.
Fatma mwenye umri
wa miaka 54 amefanya kazi umoja wa mataifa kwa miaka 21 na ataanza kazi katika
shirikisho la mpira wa miguu duniani mwezi June.Akinukuliwa Rais wa FIFA bwana
Gianni Infantino amesema “Ni muhimu FIFA kuchukua mtazamo mpya katika juhudi za
kuendelea kuijenga upya taasisi hii”.
“Amedhihirisha
pasi shaka uwezo wake wa kuongoza na kujenga timu imara ya kazi na kuboresha
taasisi hii katika utendaji wake.Kwa upande wa FIFA anaelewa vizuri kuwa
inahitaji uwazi na uwajibikaji ambao ndio moyo wa Taasisi yoyote inayofanikiwa”
alimalizia.
Hongera bi Fatma.
0 comments:
Post a Comment