Mabilioni Ya AY Na MwanaFA Hatihati Kuyeyuka Wakati Wowote


Kufuatia wanamuziki Ambwene Yesaya  (AY) na mwenzake Hamisi Mwinjuma (MwanaFA) kuamuriwa na mahakama ya Wilaya ya Ilala kulipwa bilioni mbili na kampuni ya MIC (tigo) ,kampuni hiyo imekata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu mfawidhi wa mahakam hiyo Juma Hassan.

Wanamuziki hao walioishtaki kampuni hiyo kwa kutumia nyimbo zao “Dakika moja” na “Usije mjini” kama miito ya simu bila idhini yao waliamuriwa kulipwa fidia ya shilingi milioni tano kama faini ya uharibifu lakini pia shilingi bilioni 2.16 kama faini ya jumla.

Kampuni hiyo ya tigo  kupitia mawakili wao wanaosimamia kesi hiyo wa Law Associates iliweka sababu za kukata rufaa hizo ambazo ni:

1/.Hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata

2/.Walishindwa kueleza faida ambazo wangepata kama nyimbo hizo zisingetumika kama miito ya simu

3/.Hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na badala yake kwenye kesi ya msingi waliwasilisha barua ya Basata na si cheti cha COSOTA.

Wasanii hao bado wametoa msisitizo kuwa sasa ni wakati wa muziki na kazi za wasanii kuheshimiwa na kuchukuliwa kama ajira nyingine zinazotakiwa kulindwa na kuheshimika kisheria.

 

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment