Ni ajabu ila ni
kweli.Ufilipino waamua kumchagua bi Geraldine Roman kuwa mbunge wao wa bunge la
Congress. Bi Roman ambae alizaliwa akiwa na jinsia ya kiume ila akaamua kuishi
ujinsia wa kike na kuolewa juzi alichaguliwa kwa asilimia 62 kuwakilisha jimbo
la Bataan kaskazini mwa jiji la Manila Ufilipino.
Bi Roman mjuzi wa lugha
na mwandishi wa habari,mtoto alietoka katika familia ya wanasiasa akilirithi
jimbo hilo kutoka kwa mamaye ameahidi kuendeleza kazi za kuitumikia jamii
alizozianzisha mama yake lakini pia kusaidia kutetea makundi ya jamii
yanayokandamizwa.
Baada ya ushindi huo
alinukuliwa akisema “Siamini kama ingefika siku moja mtu wa hali kama hii yangu
angechaguliwa kuingia bungeni. Hii ni salamu za kwanza kuwa hata watu
wanaobadili ujinsia wao kuwa wanaweza kulitumikia taifa na hawapaswi
kukandamizwa”.
Jinsia
na Ujinsia ni nini”?
Wataalam wanasema...
Jinsia ni ile hali
unayopewa na jamii kwa kuzaliwa hasa kutokana na kiungo cha siri unachozaliwa
nacho.Kama utazaliwa na kiungo cha kiume ama kike basi utaitwa mwanaume ama
mwanamke.
Ujinsia ni ile hali
unayojisikia kutokea ndani.Yaani tabia zinazoambatana na wewe na ile hali
unayojisikia.Unaweza ukazaliwa na jinsia ya kiume lakini ukawa unasukumwa kuwa
na tabia za kike ama kinyume chake.
Kubadili ujinsia ni tofauti
na kubadili jinsia.Unaweza ukabadili jinsia huku ukabaki na ujinsia wako ama
kinyume chake
Roman yeye alizaliwa na
kiungo cha uzazi cha kiume lakini akawa anasukumwa kuuishi uanamke hivyo
akaamua kujitangaza hadharani na kuishi kama mwanamke japo hana kiungo cha
uzazi cha kike.
Bado kuna malumbano
makali kama hizi dhana mbili ni asili ama mtu hujitakia tu kwa sababu za
kijamii.
0 comments:
Post a Comment