Pamoja na kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya mwanamke lakini pia ni vizuri kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za mwanamke kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini, vitamini na keratin na siyo rangi na vipodozi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha, inashauriwa kula mboga za majani, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.
Je! Unafahamu kuwa kucha zako zinaweza kukujulisha kuhusu afya yako? Zinaweza kukujulisha tatizo katika ini, mapafu na hata moyo wako. Tumekuwekea hapa maelezo ya kutosha ya namna muonekano wa kucha zako unavyoweza kukujulisha kuhusu afya yako.
1. Pale Nails
Pale Nail |
2. White Nails
Ukiwa na kucha rangi nyeupe alafu zimezungukwa na weusi inasemekana utakuwa na tatizo la ugonjwa wa Ini (Hepatitis). Pia inaweza kuwa ni tatizo la figo au ukosefu wa virutubisho mwilini hasa Protini.
3. Yellow Nails
Endapo kucha zako zikiwa na muonekano wa rangi ya njano basi utakuwa unatatizo la fangasi kwani ndiyo chanjo kikuu cha kucha kuwa za njano. Lakini pia unaweza kuwa na tatizo la Tezi. Tafiti zinaonesha kuwa Tezi hili la shingoni husababisha kucha kutokuwa na afya zuri kwani thyroid homoni zinasababisha kucha kutengana na ukuta (mzizi wake) hivyo kupelekea kucha kushindwa kukua vizuri matokeo yake muonekano wa kucha unakuwa ni kama kwenye picha.
4. Bluish nails.
Ublue katika kucha nalo ni tatizo, hii inawezekana ukawa na tatizo katika mfumo wa hewa. Kuwa na kucha za rangi ya blue ni matokeo ya ukosefu wa oxygen katika kucha zako. Hii inasababishwa na kuwa na mzunguuko mdogo sana wa damu hasa katika maeneo ya baridi sana. Kuwa na mzunguuka mdogo wa damu kunasabosha damu isifike katika maeneo yote ya mwili kwa kiasi kinachohitajika.
5. Rippled nails.
Endapo utaona kucha zako ziko na vidoti vidoti kama inavyonekana kwenye picha na ngazi chini ya kucha inaonekana kama nyekundu basi wewe utakuwa na dalili za mwanzo za fangasi katika ngozi (Psoriasis). Hii inasababisha seli za ngozi ya juu kufa. Mara nyingi Psoriasis inatokea kwenye ngozi, kucha, viwiko (elbow) na magoti.
6. Dark lines beneath the nails.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa endapo kucha zako zikionesha mstari mweusi kama ilivyokwenye picha, fanya haraka kutafuta hospitali kwa vipimo zaidi. Kuwepo kwa mstari huo mweusi ni dalili tosha za melanoma (Moja ya kansa mbaya sana za ngozi)
Inashauriwa kuwa ili tuweze kugundua rangi hii basi tusiwe tunapaka rangi za kucha kila mara. hii itatusaidia kutofautisha kati ya rangi za kucha na mstari huo. Vile vile kucha zikipata mwanga wa jua inakuwa rahisi kugundua rangi hizo na mwanga wa jua huwa haupiti kama kucha imepakwa rangi.
HITIMISHO.
Muonekano wa kucha ni njia rahisi kutambua afya yako lakini wakati mwingine si kila mwenye kucha nyeupe sana basi atakuwa na tatizo la ini. Pale unapohisi tu muonekano wa kucha zako umekuwa tofauti na ulivyouzoea basi fanya mpango wa kumuona daktari kwa ushauri na uangalizi zaidi.
Kwa afya njema ya kucha, mwanamke pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni. Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus) wanaoshambulia kucha.
Imeandaliwa na Muhsin Hero.
0 comments:
Post a Comment