Mfanya biashara tajiri na mmiliki wa timu kali ya
mpira wa miguu ya TP Mazembe MOISE Katumbi jana alitangaza rasmi kuwania kiti cha
urais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Gavana huyo wa zamani wa jimbo la
Katanga na mmiliki wa migodi kadhaa ya dhahabu ameweka wazi nia yake hiyo huku
akimuonya Rais Joseph Kabila kutoingiza nia ovu ya kutaka kugombea tena
madaraka kwa kuichakachua katiba ambayo kwa sasa haimruhusu kufanya hivyo.
Kuna tetesi kuwa Rais Kabila yupo kwenye mpango
kabambe wa kutaka katiba ibadilishwe ili aweze kugombea tena Urais jambo ambalo
Katumbi amesema linaweza kusababisha machafuko makubwa. Katumbi anaetarajiwa
kuendesha kampeni nzito kutokana na uwezo wake wa kifedha tayari amaeshaanza
kuwa tishio na kwa chama kinachotawala sasa maana tayari vyama kadhaa vya
upinzani vimeshatangaza kumuunga mkono. Ametangaza kugombea nafasi hiyo kama
mgombea binafsi.
Katumbi amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini
ya chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae
akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka hu 2016 amekuwa akitoa kauli
zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo mtaka kustaafu mwishoni
mwa mwaka huu.
Licha ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni
uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo
tangu kujiuzulu kwake 2015.
Uchaguzi huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa
Katumbi ana nguvu kubwa ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na
katika ngazi ya taifa licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati
wa uongozi wake.
Wachunguzi wa habari za siasa wamesema nchi hiyo
inanyemelewa na machafuko iwapo Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa
hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.
0 comments:
Post a Comment