Baada
ya watu kumwita Rais hafuati sheria na anautawala wa kiimla leo
amewadhihirishia tena kuwa kauli hizo hazimrudishi nyuma katika kutekeleza
majukumu yake aliyokabidhiwa kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Akiwa
mjini Katesh leo Rais Dr.John Pombe Magufuli amenukuliwa akikemea vikali baadhi
ya wafanyabiashara wanaohujumu uchumi hasa katika bidhaa ya sukari iliyoleta
sintofahamu kuwa waache vitendo hivyo la sivyo wanacheza na maisha yao na kuwa
wasiporekebisha tabia ya kuficha sukari ili kusababisha upungufu wa makusudi
basi sukari hiyo ataikamata na kuigawa bure na kamwe hawatakaa wafanye biashara
Tanzania maisha yao yote.
“Nitoe wito kwa
wafanyabiashara ambao wanasukari na wameficha kwenye maghala, kuna mmoja
alienda kununua Kilombero zaidi ya tani elfu tatu halafu mpaka leo
hajaichukua. Kuna mwingine ana ghala kule mbagala kwa taarifa nilizo nazo leo
ana tani elfu nne nazo hataki kuziuza ili kusudi wananchi wakose sukari”
“Nataka niwaambie sukari
haifichiki kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola vifatilie wafanyabiashara
wote ambao wameficha sukari wale ni wahujumu uchumi tutachukua sukari ile na
kuigawa bure. Tutaichukua sukari na hawatakaa wafanye biashara maisha yao yote
hapa Tanzania, kwa hiyo kama wapo wafanyabiashara wanaotaka kunijaribu na
kucheza na serikali wajue wanachezea maisha yao. Waitoe hiyo sukari wakauze kama
walivyokuwa wamepanga” alimalizia.
Ikumbukwe
nchi sasa hivi ipo kwenye sintofahamu ya upungufu wa sukari mara tu baada ya
Rais kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje ambapo baadae serikali kwa
kupitia waziri mkuu iliruhusu tena uingizwaji huo.
0 comments:
Post a Comment