Sasa
imethibitishwa kuwa mgombea anaewania kuteuliwa na chama chake kupeperusha
bendera ya Democrats katika uchaguzi ujao wa Marekani Bi Hilarry Clinton
anatarajiwa kuhojiwa vikali na taasisi ya upelelezi ya Marekani FBI juu ya
sakata lake la kujiundia barua pepe nyumbani kwake na kuitumia kwa mawasiliano
ya ofisi alipokuwa Mtendaji mkuu wa serikali wakati wa awamu ya kwanza ya
Obama.
Mmoja wa wasaidizi
wake wakuu Huma Abedin tayari ameshahojiwa na FBI katika ofisi zao za
Washngoton mwezi April. FBI na idara ya sheria ya Marekani wamekuwa wakifuatilia
na kupeleleza iwapo kuna taarifa zozote nyeti ambazo ziliingia kwenye server ya Clinton na kutumika
vibaya. Uchunguzi huu wa FBI kwa mara ya kwanza uliripotiwa mwezi August mwaka
jana. Bado haijajulikana uchunguzi huu utachukua muda gan lakini wasaidizi wa
Clinton katika kampeni wamesema wanahakika uchunguzi huu ukimalizika basi
itabainika kuwa hakuna lolote baya lililokuwa limetokea.
Clinton amekiri
kuwa jambo alilofanya lilikuwa ni kosa japo alisisitiza kuwa hakupokea nyaraka yoyote iliyokuwa siri wakati huo. Uchunguzi mpaka sasa unaonyesha kuwa
server yake ilipokea nyaraka ambazo zilikuwa ni zaidi ya siri japo mwenyewe
amekataa kata kata jambo hilo.
Sakata hili
linampa nafuu kidogo Bernie Sanders anaeonekana kulemewa na mpinzani wake huyo
ndani ya chama. Kama Bi Hilarry akionekana na makosa sakata hilo laweza
mpunguzia nafasi ya kumshinda mpinzani wake Bernie Sanders.
0 comments:
Post a Comment