Ferdinand Wambali Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora
anatarajiwa kutoa hukumu ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma
Kusini kesho tarehe 17 Mei.Katika kesi hiyo iwapo David Kafulila aliyekuwa
mgombea wa kiti cha ubunge kupitia NCCR-Mageuzi atashinda basi ataruingia
bungeni rasmi.
Kesi
hiyo ya kupinga matokeo ilifunguliwa na David Kafulila aliyekukuwa mgombea wa
ubunge katika jimbo hilo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi dhidi ya mpinzani wake
Husna Mwilima wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayedaiwa kupoka ushindi wa
Kafulila.
Wambali anayesimamia kesi hiyo katika taarifa yake
iliyotolewa siku ya jumatano tarehe 4 mwezi huu mjini Tabora amesema kuwa, amepanga
kutoa hukumu kesho baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo
yao
Awali, Jaji Wambali aliamuru Mwilima kuwasilisha
ushahidi uliompa ushindi lakini pia msimamizi wa uchaguzi huo naye apeleke
ushahidi uliomfanya ampe ushindi Mwilima.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Wambali aliomba
kupatiwa muda wa kutosha ili kupitia ushahidi huo na vielelezo
vilivyowasilishwa ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila
anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi mpinzani
wake Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa
jimbo hilo kwa mujibu wa kura zake.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na, Mbunge wa
jimbo hilo, Mwilima , Mfaume, na Mwanasheria wa serikali anayewakilisha Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ktika kesi hiyo wakili Kenedy Fungamtama anamtetea
Mwilima huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu Prof. Abdallah Safari,Tundu
LissU na Daniel Rumenyela.
0 comments:
Post a Comment