Aliyekuwa
Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue sasa amestaafu bila kupangiwa kazi
nyingine kama alivyoahidiwa na Rais John Magufuli siku aliyomteua Balozi
Injinia John Kijazi kushika wadhifa huo na hivyo Balozi Sefue kutolewa kwa
madai ya kupangiwa kazi nyingine.
Tarehe
6 mwezi Machi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
alimteua John William Kijazi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu kiongozi wadhifa
ambao hapo kabla ulikuwa ukishikiliwa na Balozi Ombeni Sefue.Balozi Sefue
alieteuliwa tena na Rais Magufuli Desemba 20, 2015 kuendelea kushika wadhifa
huo kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya utumishi wake wa umma kuisha sambamba
na makatibu wakuu na manaibu 50.
Katika
uteuzi ule wapo makatibu wakuu na manaibu walioachwa akiwemo Dkt.Donald Mbando
(Afya),Balozi Liberata Mulamula (Mambo ya Nje), Omari Chambo (Nishati na
Madini), Jumanne Sagini(Tamisemi) na Joyce Mapunjo (Afrika ya Mashariki).Balozi
Sefue alirudishwa tena lakini ghafla Machi 6 alisimamishwa na kumpisha Kijazi
kwa maelezo kuwa atapangiwa kazi nyingine.
Lakini
sasa imethibitika kuwa Balozi Sefue hatapangiwa kazi nyingine na kwamba muda
wake wa kustaafu ulifika na hivyo hawezi kuendelea tena na utumishi wa
umma.Akijibu maswali ya mwandishi wa gazeti la Mwananchi juu ya hatma ya
makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu walioahidiwa kupangiwa kazi nyingine
,Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Dkt Laurean Ndumbaro
alisema kuwa makatibu wakuu wote wamepata barua zao na hakuna ambae hana kazi
isipokuwa kwa wale waliostaafu kwa mujibu wa sheria kama Balozi Sefue, Balozi
Mulamula na Chambo ambao hana uhakika kama wanaweza kupangiwa majukumu mengine.
Swali
ni je kama aliongezewa mwaka mmoja wa mkataba katika utumishi wa umma
alipotolewa kwenye nafasi ile mara baada ya ueuzi kutenguliwa na Kijazi
kuchukua nafasi yake mkataba wake ulivunjwa?Kama haukuvunjwa analipwa mshahara
mpaka sasa kwa kazi gani anayoifanya?Kama ulivunjwa je Rais alimdanganya?.
0 comments:
Post a Comment