Orodha Ya Makundi Kumi Hatari Zaidi Ya Kigaidi Duniani


Ugaidi upo,ni ukweli pasi shaka kuwa upo na Dunia haina budi kutafuta jitihada zozote kupapambana nao.Hii ni orodha ya makundi hatari na mabaya zaidi ya kigaidi duniani.
10. The Lord’s Resistance Army (LRA)
The lord’s Resistance Army  ni kundi la kigaidi linalofanya shughuli zake sehemu kadhaa za Uganda, Jamuhuri ya Afika ya Kati na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sehemu baadhi ya Sudani ya Kusini.Kiongozi wake anaita Joseph Kony.
 9. Forças Armadas Revolucionárias da Colômbia (FARC)
Ukitafsiri kwa Kiswahili linaitwa Jeshi la kimapinduzi la Colombia.Linasemekana kuundwa  kipindi cha ugomvi kati ya chama cha wahafidhina na waliberali huko Colombia.Ni kikundi hatari sana.
 8. Tehrik-e Taliban Pakistan
Kundi hili limeundwa na waislam wenye itikadi kali wa mpaka wa Pakistan na Afghanistan na lengo lao kubwa ni kuipindua serikali ya Pakistan, kupigana na majeshi ya NATO yaliyoko Afghanstan na kuweka utawala wa sharia kama sharia pekee Afghanistan.Kiongozi wake wa sasa anaitwa Mullah Fazlullah.Kundi hili lina mashirikiano ya karibu sana na Al-Qaeda.Kiongozi wa kundi hili ndiye aliemuua Benazir Bhuto aliewahi kuwa waziri mkuu wa Pakistan.Kama hujaisoma habari hii ipo hapahapa kwenye blog hii yenye kichwa cha habari “Huyu ndiye aliyemuaa Benazir Bhuto…” http://tiadventurers.blogspot.com/2016/05/huyu-ndiye-aliyemuua-benazir-bhutto.html
 7. Lashkar-e-Tayyiba
Lashkar-e-Tayyiba (LT)  ni kundi la kigaidi lenye maana ya Jeshi la wenye haki.Linafanya shuguli zake za kigaidi Pakistan na India na limekuwa na sifa ya kuwa jeshi lenye wapiganaji mahiri na kubwa Zaidi eneo hilo. Lilianza kama sehemu ya jeshi ya Markaz-ud-Dawa-wal-Irshad mapema 1900s,likiwa ni kundi la kiislamu lenye kupinga uwepo wa umoja wa Kirusi nchini Afghanistan.
 6. Al-Shabaab
Kundi maarufu ukanda huu wa Afrika Mashariki lililoanzishwa mwaka 2006 lenye lengo la kutoa vikosi vyote vya nchi za kigeni Somalia na kusimika serikali ya kiislamu.Linafanya shughuli  zake Somalia,Kenya, na Uganda. Baadhi ya mashambulizi yao mabaya ni lile la mwaka 2013 pale Westgate Kenya ambapo watu 60 walipoteza maisha yao na pale Chuoni Kenya ambapo wanafunzi 148 walikufa mwaka 2015.
 5. Hezbollah
Hezbollah lenye maana ya Chama cha Mungu ni kikundi cha kijeshi kinachoisha makali yake lakini bado kina nguvu.Ni kikundi kilichoanzishwa na viongozi wa ngazi za juu wa kiislamu na kikaja kuwa kikundi kinachopingana na Israel  kuikalia Lebanon miaka ya 1982. Leo kikundi hiki kina muwakilishi katika serikali ya Lebanon na hivyo hakitajwi tena kwenye vyombo vya habari kama kikundi cha kigaidi.
 4. Boko Haram
Boko Haram ni kundi baya kabisa na hatari Zaidi Afrika lililopo nchini Nigeria na lenye mashirikiano ya karibu kabisa na Al-Qaeda.Mwanzilishi na kiongozi wake anaitwa  Mohammed Yusuf, na chini ya uongozi wake amefanikiwa kufanya mauaji ya watu wasio na hatia 5,000 na kuteka watoto 200 wanafunzi wa kike huko Nigeria na linatishia kuipindua serikali ya Nigeria.
 3. Taliban
Taliban lilianzishwa na  Mullah Mohammed Omar,  huyu mpaka leo anabaki kuwa kiongozi mkuu wa kiroho wa kundi hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994. Taliban ni moja ya makundi hatari zaidi kwa ugaidi na ni namba tatu duniani.
 2. ISIS
ISIS  ni kifupisho kinachosimama badala ya  Islamic State of Iraq and al-Sham  ,kundi hili linakuwa kwa kasi ya ajabu na linakuwa ndio kundi hatari Zaidi duniani kwa ugaidi likishikilia namba mbili linakadiriwa kuwa na idadi ya wapiganaji takribani 80,000.
 1.Al-Qaeda
Kundi hili ndilo linashikilia nambari moja.Habari za kundi hili zinajulikana kila mahali kwa kila mtu hata hapa Tanzania walishatufanyia tukio katika ubalozi wa Marekani.Kundi hili ni hatari zaidi kuliko yote uliyowahi kuyasikia.Lina teknolojia ya hali ya juu na mtandao usiomithilika.
(Orodha hii ni kwa msaada wa mashirika ya habari kama bbc.com, theatlantic.com, pbs.org, warchild.org, nctc.gov and The Richest)
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment