5.1 Mkataba tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali , ilihoji
utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya Mfumo wa Alama za Vidole (AFIS)
ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
Mheshimiwa Spika, kumetokea majibishano na malumbano mengi kwenye vyombo
vya habari na miongoni mwa wabunge wa Bunge lako tukufu, hasa pale walipoanza
kuhoji utekelezaji wa mkataba huo hasa kuhoji juu endapo vifaa hivyo vinafanya
kazi.
Mheshimiwa Spika, Kufuatia majibishano na malumbano yaliyojaa utata ambao
lazima upatiwe majibu yasiyo na shaka yoyote, hivyo basi, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kutoa majibu ya moja kwa moja bila kupepesa
macho. Tunataka Maswali yafuatayo yajibiwe hapa bungeni;
Mheshimiwa Spika,
1)
Kwa kuwa mikataba ya serikali kwa mujibu wa sheria lazima ufuate sheria za
manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Je, Utaratibu
huu ulifuatwa?
2)
Je Mkataba huu wa LUGUMI ENTERPRISES na JESHI LA POLISI umetekelezwa ama
haukutelezwa, na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikua na
tatizo la utekelezaji, Je, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?
3)
Je, ni kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati
ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa kampuni ya INFOSYS ambayo
mmoja wa wamiliki wake ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Charles
Kitwanga inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS).
4)
Ni kwanini C.A.G katika ukaguzi wake hakuhoji kuhusu uhalali na ulinganishi wa
thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa hivyo?
5)
Kampuni ya INFOSYS (inayomilikiwa na Mhe. Kitwanga) imedai kulipwa na Jeshi la
Polisi, takribani Dolla za Marekani 74,000, Je fedha hizi Kampuni ya Mhe.
Kitwanga ililipwa kwa kazi ipi iliyofanya na Jeshi la Polisi?
6)
Ni kwanini mpaka sasa , Rais Magufili hajachukua hatua dhidi Said
Lugumi, na aliyekuwa IGP Said Mwema / Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani na kuwasimamisha kazi wale wote ambao bado wako
kazini juu ya mkataba tata wa Lugumi ?
7)
Tunamtaka Rais , kutengua mara moja uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani Mathias Chikawe na kumrudisha nchini mara moja , kwani alihudumu kama
Waziri wa Mambo ya Ndani na ni imani ya Kambi rasmi kuwa alijua mambo yote
yanayoendelea ya mkataba wa Lugumi
Mheshimiwa Spika , Ni imani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa
Mhe.Waziri Charles Kitwanga, anazo taarifa za Mkataba huu na utekelezaji wake
aidha kutoka kwenye Kampuni yake ambaye yeye ni Share holder ( Mbia ) ambayo
ilifunga vifaa hivi au anazo taarifa ya utekelezaji wa Mkataba huu kutoka Jeshi
la Polisi ambalo liko chini yake kwa kiwango chote kuhusu mambo yote ya Mkataba
huu.
Mheshimiwa Spika, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) ,
alinukuliwa na vyombo vya habari pale alipoulizwa kuhusu sakata la Lugumi na
Mikataba yake na Jeshi la Polisi kutotekelezwa, alijibu majibu mafupi Katika
gazeti la Raia Mwema la tarehe 27/04/2016 namnukuu “siyo kweli, watu wana
ugomvi wao kibiashara, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote
tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa
sababu ya kukosekana kwa internet” Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, kulingana na maswali ambayo tumeuliza hapo juu na
uchambuzi wetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kama ifuatavyo;
Mheshimiwa Spika,
1. Kwa vile Waziri wa Mambo ya Ndani anahusika kwa karibu
katika Mkataba huu kupitia Kampuni yake ya INFOSYS na vile vile Jeshi la Polisi
liko chini yake , je ? haoni kuwa ni busara kwa yeye kujiuzulu ili kutoa nafasi
ya Uchunguzi kuepusha mgongano wa maslahi ndani ya Jeshi la Polisi na kwenye
Kampuni ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki ?
Mheshimiwa Spika,
2.
kwa vile
inaonekana kupitia vyombo vya habari na kauli za viongozi mbali mbali kuwa upo
uwezekano wa Polisi kuwa wametapeliwa na vifaa hivyo havijafungwa, Kambi ya
Upinzani Bungeni inautaka uongozi wote wa juu wa Jeshi la Polisi kujiuzulu mara
moja, kwani kama wao wameshindwa kujua ukweli wa vifaa vilivyofungwa kwenye
vituo vyao vya Polisi ama vipo au havipo, watawezaje kuchunga na kulinda mali
na usalama wa raia wengine?
Mheshimiwa Spika,
3.
Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, inataka majibu yote yanayohusu Mkataba wa Lugumi na Jeshi la
Polisi kuhusu utekelezaji wake uwekwe wazi hapa bungeni na wizara husika.
0 comments:
Post a Comment