Kwa mujibu wa watafiti, Waingereza “…ndio watu
wenye ubinafsi zaidi duniani, ndiyo jamii inayokazia zaidi faida za kibinafsi
kuliko watu wa nchi nyingine yoyote duniani,” likaripoti gazeti Daily
Telegraph la London, Uingereza.
Uchunguzi mwingine ulionyesha kwamba Waingereza
wanapatwa na huzuni na mifadhaiko kuliko raia wa taifa jingine lolote duniani.
Wataalamu fulani wanaamini kwamba mambo hayo mawili—ubinafsi na
huzuni—yanahusiana.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha
Northwestern kilichoko Chicago, Marekani, ulilinganisha jamii mbalimbali
duniani, kama zile zinazopatikana katika nchi za Ulaya, na zile za China na
Taiwan.
Ilionekana kwamba kwa kuwa jamii za China na
Taiwan zinathamini zaidi ushirikiano katika jamii badala ya ubinafsi, watu wanalindwa
wasipatwe na matatizo ya kiakili.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
mwanasaikolojia wa Uholanzi, Geert Hofstede, imegundulika kuwa katika nchi
zilizo na jamii zenye watu wabinafsi zaidi, Uingereza ilishika namba moja
katika orodha, ikifuatiwa na Marekani, Australia na nchi nyingine za Magharibi.
Katika nchi za Ulaya, “jamii yenye ubinafsi …
inatufanya tuhuzunike,” linasema gazeti Telegraph.
Hata hivyo, kiwango cha huzuni na mfadhaiko
katika jamii hizo ni cha juu sana kuliko mahali pengine popote duniani, kwa
mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliojulikana kama
‘Depression: A Global Public Health Concern’.
“Tumegundua uhusiano wa ajabu sana kati ya
ubinafsi, huzuni na mfadhaiko,” anasema Dk. Joan Chiao, mwandishi wa taarifa ya
utafiti huo, na kuongeza, “Mataifa yenye watu walio na
ubinafsi zaidi wameonyesha kiwango cha juu sana cha huzuni na mfadhaiko.”
“Kiasi cha mmoja kati ya watu 10 nchini
Uingereza anateswa na ama huzuni au mfadhaiko ikilinganishwa na mmoja kati ya
watu 12 katika Bara la Ulaya,” likaandika gazeti Telegraph na kuongeza
hivi: “Inakadiriwa kuwa kiwango cha mfadhaiko na huzuni nchini China ni kiasi
cha mmoja kati ya watu 25.”
0 comments:
Post a Comment