Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise
Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha
sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya
dola milioni 6.
Katumbi hakuwa
mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika
kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa
kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa
kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa
hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya
kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.Amesema atakata rufaa
Nini Chanzo Cha Hii Figisufigisu?
Wapinzani na wafuasi
wa Katumbi huko Congo wanaiona hii kama komoa komoa ya Rais Kabila dhidi ya
Katumbi ambapo hapo kabla walikuwa maswahiba.Uswahiba wao ulianza kuingia doa
pale tu Rais Kabila alipotaka kulivunja jimbo la Katanga ambalo ndio kama milki
ya Katumbi kiuchumi na kiutawala liwe katika majimbo madogo madogo manne.Baada
ya kutoelewana hapo ugomvi ulianza lakini ulichagizwa zaidi baada ya Katumbi
kuona Rais Kabila hana nia ya kuachia madaraka na akatoa kauli ya kumtaka atoke
madarakani muda unapokwisha November mwaka huu.
Kukazia zaidi Katumbi
alitangaza nia yake ya kugombea urais na ndiop[o hapo vita yake na Rais Kabila
vilipamba moto.
0 comments:
Post a Comment