Kwa kawaida papa ni mtu anaefatiliwa sana.Kila anachosema,kuvaa,kutenda huwa kinachukuliwa maanani na kutafsiriwa sana.Moja ya vitu vinavyofatiliwa ni mavazi yake na aina ya vitu anavyopenda kutumia hasa magari.Leo tunakuletea magari bora 10 yaliyowahi kutumiwa na ma papa mbalimbali katika historia ya kanisa.Tutaanza miaka ya 1960 maana kabla ya hapo papa alikuwa hatembei sana nje ya vatican ama italia.
Lincoln Continental |
1.Lincoln Continental
Ni
toleo la miaka ya 1960.Mwaka 1965 papa Paul VI akiwa anatembelea Marekani kwa mara
ya kwanza papa kusafiri kwenda Marekani kampuni ya magari ya Ford iliombwa
kumtengenezea papa gari maalum.Ilipewa taarifa hizo wiki mbili kabla ya ujio
wake na ndio likaja na hilo toleo.Papa alilipenda sana na mwaka 1968
alitembelea tena na kuomba atumie gari hiyo hiyo.
Mercedece-Benz Pullman |
2.Mercedece-Benz 600 Pullman
Kati
ya mwaka 1964 – 1981 Mercedece Benz 600 ndilo lilikuwa gari la gharama kubwa
kuliko yote duniani.Lilikuwa likitengenezwa kwa oda maalum ya mnunuzi ili gari
moja lisifanane na lingine hivyo mwaka 1965 kampuni ilimtengenezea papa gari
lake lenye vigezo vyake mwenyewe.
Citroen SM Presidentielle |
3.Citroen SM Presidentielle
Hakukuwa
na gari zuri kwa ajili ya papa miaka ya 1970’s kama hili alilotumia papa John
Pual II alipotembelea Ufaransa mwaka 1974
Fiat Campaignola |
4.Fiat Campaignola
Hili
ndilo gari papa John Paul II alipigwa risasi akiwa juu yake May 13,1981.Hapo
ndipo mwanzo wa magari ya papa kuanza kuwekwa vioo vya kuzuia risasi.
Mercedece-Benz 230-G |
5.Mercedes-Benz 230-G
Baada
ya jaribio la kuuawa kwa papa ilibidi litengenezwe gari lenye kuzuia risasi
ndipo benz wakaingilia kati na kuja na gari hilo la papa.Kioo kile cha kuzuia
risasi ndio huitwa G-glass
Ferrari Mondial |
6.Ferrari Mondial
Hili
gari ni la mwaka 1988 na lilitengenezwa baada ya papa kutembelea kiwanda cha
magari ya Ferrari huko Marenello Italy.
Renault 4 |
7.Renault 4
Wakati
papa John Paul II na mrithi wake papa Benedicto XVI walipendelea magari kama
Mercede-Benz papa Fransis yeye alikuja na mambo yake.Yeye alitaka Renault 4
toleo la mwaka 1984 tena likiwa tayari lishatembea kilometa 186,000 na alitaka
kuwa anaendesha mwenyewe na sio kuendeshwa.
Hyundai Santa Fe |
8.Hyundai Santa Fe
Hili
nalo ni moja ya magari aliyotaka kuwa anayatumia.Mengine yakiwemo KIA Sedona na
Isuzu D-Max.
Jeep Wrangler |
9.JeepWrangler
Mwaka
2015 papa Fransis akitembelea Equador alionekana akiwa na Jeep akaonekana nalo
tena alipotembelea America.
Fiat 500L |
10.Fiat 500L
Akitokea
Cuba kwa ziara papa Fransis alipowasili America alitumia hii Fiat nyeusi.Ni ya
kisasa kabisa lakini dogo kidogo.
0 comments:
Post a Comment