Kila
mtu anajambo lake la kipekee hapa duniani.Binti huyu ajulikanaye kwa jina la
Alia Sabur alipata u professor akiwa
na umri wa miaka 19 tu.Kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness Book of World Records kimemwandika kuwa anashikilia nafasi
hiyo mpaka sasa.
Alia
mzaliwa wa Northport New York alijua kusoma na kuandika akiwa na umri wa miezi 8 tu.Alimaliza mtaala wa elimu
yake ya msingi akiwa na umri wa miaka 5.Akajiunga
na masomo ya sekondari huko New York katika shule bora zaidi ambayo pia
walisema hawawezi kuwa nae maana amepitiliza viwango ndipo akajiunga na chuo kikuu
akiwa na umri wa miaka 10 na
kumaliza shahada ya kwanza ya sayansi ya mahesabu chuo cha Stony Brooks akiwa
na miaka 14.Akiwa na miaka 17 alimaliza shahada ya uzamili
katika sayansi ya uinjinia na akiwa na miaka
19 tayari alikamilisha shahada ya uzamivu (PhD) na kutangazwa kama Professor mdogo kuliko wote duniani
akifundisha chuo kikuu cha Konkuk jijini Seoul Korea Kusini.
Colin Maclaurian |
Alia
anavunja rekodi iliyokuwa imeshikiliwa kwa muda mrefu sana ya Colin Maclaurian
mwanafunzi wa mwanafizikia maarufu Isack Newton aliepata kuwa professor akiwa
na umri wa miaka 19 mwaka 1717 huko chuo cha Aberdeen.
Alia
mwenye umri wa miaka 26 sasa alisema “Mara nyingine kuna kipindi cha mpito
ambacho kunatokea watu wa aina yangu wanaofanya mambo ya kipekee katika umri
mdogo lakini kadiri anavyokua anabadilika na kuwa mtu mzima wa kawaida tu asie
tena na vitu vya kipekee.Yaani upekee wake ulitokana na umri wake lakini katika
hali ya kawaida hakufanya jambo la kipekee”.
0 comments:
Post a Comment