Na:Dotto Chamchua
Leo tunaendelea na sehem ya pili ya makala yetu tunayoangazia umoja kati ya uchawi na miujiza.Tuliishia kwenye tanbihi sasa tutaendelea.
Tanbihi:
nikizungumzia asili ya kitu fulani, jua kuwa nazungumzia muumbaji wa kitu
hicho. Mungu ndiye aliyeumba “uchawi” na huo “muujiza” Uchawi na muujiza ni
viumbe wa Mungu kama vilivyo viumbe vingine, kama tikikataa kuwa uchawi na
mujiiza sio viumbe wa mungu, basi tukubali kuwa kuna “kitu” kingine tafauti na
“MUNGU” ndio kimeumba uchawi na muujiza, jambo ambalo halikubaliki katika dini
zote, yaani, hata zile za kipagani.
“Sifa
njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;” Qur-an 1:2
“Bwana
amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.”
Mithali 16:4
“Mwenyezi
Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na
akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa
Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?” Qur-an 31:4
“Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”
Yohana 1:3
Biblia Takatifu |
Katika
aya za hapo juu zote zinadhihirisha kuwa MUNGU ndiye aliyeumba viumbe vyote
ikiwemo na uchawi na nduguye muujiza. Mfano katika andiko hilo la Mithali 16:4,
Mfalme Suleiman[a.s] anatuambia kila kitu kimefanywa[kimeumbwa] na MUNGU kwa
makusudi yake, kwa vyovyote vile hata uchawi kwa siku ya uchawi na muujiza kwa
siku ya muujiza. Sitaki nijikite katika sababu zilizopelekea MUNGU kuumba
uchawi na muujiza, kwani nachelea kutoka nje ya mada, kwa ufupi naomba mridhike
kuwa MUNGU ndiye aliyeviumba vitu hivi kama nilivyothibitisha kwa kutumia
misahafu yetu.
Hivi
uchawi na muujiza unafanyaje kazi hata uweze kushinda sheria za kimaumbile? Ili tuweze kujua namna uchawi na muujiza unavyofanya
kazi, ni lazima tujue Mungu alitumia nini kuumba ulimwengu. Imethibiti katika
dini zote, hadi zile za kipagani kuwa MUNGU alitumia “NENO” katika kuumba
ulimwengu, yaani aliposema na iwe bahari, basi papo hapo na ikawa bahari.
Tunaweza kusema hiyo papo hapo ni sawa na kitendo cha kufumba na kufumbua.
“Yeye
ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi
huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa” Qur-an 2:117
“Mungu
akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu
akatenga nuru na giza” Mwanzo 1:3-4
Muda
kwa upande wa MUNGU haupimwi kwa kutegemea vitendo vifanyavyo na jua, mwezi na
dunia, bali hupimwa kwa utaratibu ambao MUNGU mwenyewe ndio anaujua. Ndio maana
Mungu alianza kuhesabu siku katika uumbaji wake hata kabla ya kuumbwa jua,
mwezi na dunia. Muda kwa upande wa kibinadamu hupimwa kwa kwa kutegemea
mzunguko wa dunia katika mhimiri wake, kitendo cha dunia kuzunguka jua na mwezi
kuzunguka dunia, kwa MUNGU ni tafauti, utafauti huu ndio hufanya siku moja kwa
MUNGU kwa binaadamu ni miaka elfu moja. Je. Kufumba na kufumbua kwa MUNGU kwa
binaadamu ni sawa na miaka mingapi?
“Lakini,
wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu,
na miaka elfu ni kama siku moja” 2 Petro 3:8
“
Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama
kesha la usiku.” Zaburi 90:4
Hii
ina maanisha nini? Hii ina maanisha kuwa “NENO” lina nguvu na kasi ya ajabu
katika utekelezaji wa majukumu yake, jambo ambalo limefanywa kwa siku moja na
“NENO” litatugharimu miaka elfu sisi kulifanya, tena kwa vyovyote vile katika
kipindi chote cha hiyo miaka elfu moja itatupasa tuache kufanya kila kitu,
yaani hata kula, na kisha tujikite katika utafiti. Je, yupo mwenye uwezo kuishi
miaka elfu moja kwa kufanya utafiti tu? Kutokana na sababu hii ndio maana
nasema ni vigumu kwa mja kuzikiuka sheria za kimaumbile ili hali yuko mwenyewe.
Pamoja
na ugumu huo, lakini waja wangali wanazikiuka sheria za kimaumbile kila uchao.
Wanazikiuka sheria hizi si kwa kutumia uwezo wa kibinaadamu, bali inawapasa wawe
zaidi ya binaadamu wakati wakizikiuka sheria hizi, kinyume chake kamwe
binaadamu hawezi. Kwakuwa ulimwengu na sheria za kimaumbile zimeumbwa na MUNGU
kwa kutumia “neno” basi binaadamu hulazimika kutumia “neno” wakati akitaka
kukiuka sheria za kimaumbile.
“Yesu
akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake
ukatakasika” Mathayo 8:3
TB Joshua muhubiri na mfanya miujiza maarufu |
Nataka
“takasika” hilo neno nililoliwekea funga na fungua semi ndio neno lilotumika
kumponya huyo mtu mwenye ukoma. Ili neno lipate kukiuka sheria za kimaumbile ni
lazima liwe na pumzi ya MUNGU aliye hai; Hivyo neno hilo “takasika” lilikuwa na
pumzi ya mungu wakati ule linatamkwa na Yesu Kristo, na ndio maana likaweza
kukiuka sheria za kimaumbile na hatimaye likasababisha muujiza wa kuondoa ukoma
katika mwili wa mhitaji. Hata wachawi hutumia “neno” lenye pumzi ya mungu
wakati wakifanya mambo yao ya kichawi, sema wao wanatumia neno hilo pasina
kupewa kibali au ruhusa na mungu.
Pamoja
na kwamba “neno” ndio kila kitu katika shughuli za kimuujiza na kichawi, lakini
haindoi ukweli kuwa kuna vitu vingine hutumika pamoja na neno katika
kukamilisha mambo ya kichawi na ya kimuujiza. Kikubwa mfanyaji uchawi au muujiza
ni lazima ajue anataka kufanya nini, kwa wakati gani, kwa nani na vitu gani
vitahitajika katika kukamilisha huo muujiza au uchawi.
Labda
niseme kitu kimoja “nyakati” na “idadi" ya vitu, mambo, vitendo au matukio
katika shughuli za kichawi na muujiza ni muhimu sana, usipojua matumizi sahihi
ya vitu hivyo inawezekana uchawi au muujiza wako usifanikiwe, au usifanyike
kama vile ambavyo ulivyotaka.
“Alipokwisha
kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu
tope za macho, akamwambia, Nenda kanawe
katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi
anaona”
Kwa
vyovyote vile Yesu Kristo aliona kuwa pindi akitumia “neno” tupu pasina tope
lililotokana na udongo na mate yake, yule mtu asingepona ukoma aliokuwa nao.
Katika andiko hilo halionekani neno lenye pumzi alilolitumia Yesu Kristo,
lakini haiondoi ukweli kuwa alitumia neno pia; kwa maana nia ya kutaka uponyaji
ujengwa na “neno” ndani ya moyo, na Yesu alikuwa na nia ya kutaka kufanya
muujiza. Nia ambayo kimsingi ndio “neno” katika muktadha huu sanjari na tope
ndio vilivyowezesha kukamilisha tukio la muujiza.
“Nawe,
mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe
juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia,
ukazigawanye nywele hizo. Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku
za mazingiwa zitakapotimia; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande
zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma
yake. Nawe twaa nywele chache katika hizo, na kuzifunga katika upindo wa mavazi
yako. Nawe utatwaa tena baadhi ya hizo,
na kuzitupa katikati ya moto, na kuziteketeza katika moto huo; kutoka nywele
hizo moto utakuja na kuingia katika nyumba yote ya Israeli” Ezekieli 5:1-4
Koran Tukufu |
Katika
aya za hapo juu Mungu anamwambia nabii Ezekieli afanye mambo hayo ili apate
kuuchoma moto nyumba za watenda maovu katika Israeli kwa kutumia muujiza.
Katika kutekeleza huo muujiza, Ezekieli aliambiwa afanye yafuatayo, aliambiwa
awe na upanga, kisha kwa kutumia huo upanga anyoe nywele na ndevu. Swali la
kujiuliza, kwanini Mungu alitaka atumie upanga kunyolea hizo nywele na ndevu
badala ya wembe ambao ndio kitu makhususi kwaajili ya kunyolea? Kwa vyovyote
vile kama ungetumika wembe huo muujiza usingekuwa kama vile alivyotaka Mungu.
Kisha
akaambiwa hizo nywele na ndevu azigawe katika mafungu matatu kisha na azifanye
kama alivyoambiwa. Yaani zingine azitupe kwenye maji[sijui kama aliambiwa mtoni
au baharini], zingine azipeperushe kwa kutumia upanga, na zingine katika fungu
la tatu kidogo azifunge katika upindo wa vazi[hirizi] na zingine azichome moto.
Pindi akitekeleza mambo haya basi nyumba za waovu katika Israeli zitashika
moto. Kwanini Mungu alitaka nabii Ezekieli afanye yote haya badala ya kutumia
neno tu? Hapo ndipo utakapogundua kuwa muujiza wakati fulani hauwezi kutimia kwa
kutumia “neno” tu.
Hata
uchawi nao hutumia “neno” na baadhi ya vitu vingine, na hii inategemea na huyo
mchawi anataka kufanya nini, kwa nyakati gani na kwa nani. Kuna baadhi ya mambo
ya kichawi yanafanikiwa pindi yakifanyika mchana kuliko hata usiku, mengine
yanataka saa maalumu , mengine yanataka mahali maalum, mengine yanataka mavazi
maalum na mengine yanataka matukio maalum, kwa mfano siku ya tukio la kupatwa
jua au mwezi kuna baadhi ya mambo ya kichawi yanataka yafanyike siku ya matukio
hayo. Aya ya hapo chini inatujilisha ni kwa namna gani baadhi ya vitu hutumika
pamoja na “neno” katika kutimiza mambo ya kichawi.
“Useme,
Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo
vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za
watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?”
Ezekieli 13:18
Kumbuka
kuwa nilisema anayefanya uchawi hufanya hivyo kwa kutumia "neno"
lenye pumzi ya Mungu pasina kupewa kibali na Mungu mwenyewe. Yale mambo
aliyoyafanya Ezekieli anaweza kuyafanya mtu mwingine na akafanikiwa kutimiza
kama alivyofanya Ezekieli. Ni kawaida sana kwa wachawi kutumia nywele, kufunga
hirizi, kuchoma mafusho, kutupa vitu baharini au mtoni, kuchinja wa nyama, na
mambo kadha wa kadha katika kutekeleza shughuli zao za kichawi.
Kwanini
wachawi wanaroga? ipi tiba ya uchawi? Kwanini Yesu alilazimika kumponya kipofu
kwa kutumia tope? Kuna uhusiano gani kati ya jini na uchawi? Kuna uhusiano gani
kati ya uchawi na biblia? Kuna uhusiano gani kati uchawi qur-an? Kuna uhusiano
gani kati ya uchawi na Mungu? Kuna uhusiano gani kati ya majina yetu na
uchawi/muujiza?
(Makala hii itaendelea)
Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
ReplyDelete