Wakati
Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli akisisitiza kuwa nchi za kiafrika ni
lazima sasa zijipange ili zijitegemee Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya
Kikwete jana amesema hilo haliwezekani na kuwa ni lazima nchi za kiafrika
zijipange na kujiwekea utaratibu wa namna ya kupokea misaada kutoka nchi za
ulaya kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.
Kikwete
aliekuwa akifungua mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya umoja
wa Mataifa yanayohusu “Maendeleo Endelevu kwa mwaka 20130” amesema nchi za
ulaya kutupa sisi nchi za kiafrika misaada ni jukumu lao la kihistoria maana
walitutawala na kuendeleza nchi zao kwa kutumia rasilimali zetu hivyo wanao
wajibu wa kuturudishia kwa njia za kimisaada.
Swali
ambalo wachambuzi na wataalamu wanajiuliza ni kama kweli misaada hii
inatukomboa kama bara la Afrika ama inazidi kutupumbaza na kutubakisha
nyuma.Mwandishi wa vitabu na msomi aliebobea Profesa Dambisa Moyo katika kitabu
chake cha Dead Aid alieleza kuwa
misaada haikuwahi,haiwahi na haitakaa iwahi kutusaidia sisi kama bara la Afrika
kuendelea.
Je,Kikwete
anamfanyia ukuda Magufuli?
0 comments:
Post a Comment