Shirika
La Afya Duniani WHO limesema virusi vya Zika sasa vimeingia Afrika kwa kuanzia na Cape Verde na kuwa kuna
uwezekano wa kusambaa nchi yoyote kama hatua stahiki hazitachukuliwa.Akitoa
taarifa hiyo Mkurugenzi wa shirika hilo kwa kanda ya Afrika Dkt.Matshidisco
Moeti alisema “Taarifa hii itazisaidia nchi za Afrika kujitathmini na kuchukua
tahadhari na kuongeza utayari wao wa kupambana navyo”
Alisema
nchi za kiafrika sasa ziongeze umakini kwa mama wajawazito na kuwahimiza watu
kujikinga na mbu na maambukizi kwa njia ya ngono.Lakini akasisitiza kuwa haungi
mkono njia zozote za kupambana na virusi hivi kwa kuzuia watu kusafiri.
Mpaka
sasa watu zaidi ya 7,000 wameripotiwa kuwa na virusi hivi huko Cape verde,na
kati ya hao tayari wajawazito 180 wameshaathirika navyo.Watoto watatu tayari
washazaliwa wakiwa wameharibka ubongo.
Mpaka
pale virusi hivi vilivyothibitishwa na wanasayansi nchini Senegal ilikuwa bado
haijajulikana kama ni virusi jamii ya Afrika ama ile ya Asia iliyoikumba
Brazil.Lakini sasa imethibitishwa virusi hivi ni jamii ileile iliyoikumba
Brazil vyenye asili ya bara la Asia na kusababisha matatizo makubwa ya ubongo
kwa watoto waliozaliwa.
Mtafiti
wa Kiingereza alisema kuwa virusi vya Zika vimekuwapo Afrika kwa zaidi ya miaka
50 hivyo jamii nyingi inaweza kuwa tayari imeshajitengenezea kinga tofauti na
nchi za Amerika ya kusini ambapo ndio kwa mara ya kwanza na ndio maana wakiumwa
na mbu tu wanaathirika.
Fahamu:
Virusi
vya Zika kwa mara ya Kwanza viligundulika Afrika mwaka 1947 lakini vikiwa
havina athari yoyote na ubongo tofauti na sasa.
0 comments:
Post a Comment