Gorbachev Afunguka “Najuta Umoja Wa Nchi Za Kisovieti Kuvunjika,Marekani Walishangilia Sana”


Aliekuwa Rais wa uliokuwa umoja wa nchi za Kisovieti Mikhail Gorbachev juzi alitoa ya moyoni kwa kusikitika sana na kusema Marekani walifurahi sana kwa umoja huo kuvunjika.
Akikumbushia mwitikio wa Marekani wakati wa kuvunjika kwa umoja huo mwaka 1991 Gorbachev alisema japo Marekani ilijitahidi sana kujizuia kutoonyesha hisia zao za furaha lakini walifurahi sana kuushinda umoja huo na kuhakikisha unavunjika.
“Chini ya meza wamarekani walikuwa wakisugua mokono yao kwa furaha kuu”Alisema Gorbachev.
Rais George H.W.Bush
Ndiye aliyekuwa Rais wa Marekani mwaka 1991
“Walikuwa wakiwaza na kujisemea,’Sasa sisi ndio mabosi wa dunia’.Hawakuwa na lengo la kuisaidia Urusi kukua katika demokrasia imara.Walifikiri wataikatakata Urusi na kuwa rahisi kututawala lakini matokeo yake wameshindwa na kusababisha kupoteza imani yote tuliokuwa nayo na wao”Alisema.
Aliendelea kwa kusema kuwa Urusi mpaka leo inajisikia vibaya sana kwa umoja ule kuvunjika japo wapo viongozi wachache ambao wanahitaji umoja ule urudi.”Najuta kuwa taifa kubwa kama lile lililokuwa na uwezekano mkubwa wa kuendelea sana lilipotea ghafla.Watu wengi wa Urusi wanafikiri kama ninavyofikiri mimi kuwa hatuna haja ya kuurudia umoja ule ila tunajuta kuupoteza”Aliendelea.
“Lengo langu lilikuwa kuurekebisha sio kuuvunja”Gobachev alisema akihojiwa na mtandao wa Sputnik.Akiwa anatoa maoni yake juu ya muungano wa Crimea na Urusi mwaka 2014 alimpongeza Rais Putin na kusema hata kama ingekuwa yeye angefanya kama alivyofanya Putin.”Siku zote naungaga mkono maamuzi ya watu,watu wa Crimea walitaka kuungana na Urusi”Alisema.
Fahamu:
Umoja wa nchi za kisovieti ulivunjika rasmi mwaka 1991 wakati huo Rais wa umoja huo akiwa ni Mikhai Sergeyevich Gorbachev na Rais wa Marekani akiwa ni George H.W Bush ambae ni baba wa Rais George W, Bush
 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment