Katika kile watu
wanachokiamini kama kuteleza kwa ulimi,mwezi mmoja uliopita Rais Paul Kagame alisema
“Natamani
Rwanda ivamiwe ili niwaonyeshe.Nakufa na hofu ya kusubiri vita ambavyo haviji”.Siku
mbili baadae kituo kimoja cha polisi kilivamiwa na waasi,askari karibu 18 na
walinzi binafsi wa Rais Kagame waliuawa kwenye mapigano yale yaliyodumu kwa saa
tatu.Siku moja baadae Polisi wa Rwanda wakatangaza kwamba walidhibiti ile hali.
Alhamisi ya Aprili 28,
2016 Kagame alitembelea wilaya ya Ngoma jimbo la Mashariki akiwa katika umbo lisilo la
kawaida, alikuwa ndani ya koti la kuzuia risasi “Bullet proof jacket”kama anavyoonekana pichani. Na kutokea hapo amekuwa mara kadhaa
akionekana na makoti ya aina hiyo mbalimbali hasa anapokuwa katika shughuli
zake za kikazi maeneo ya wazi.Makoti hayo yanaosadikiwa kutengenezwa Mexico
yamebuniwa na Miguel Kaballero raia wa Colombia mwaka 2010 mwezi April.
Wachambuzi wa mambo
wanasema labda hii inatokana na hofu kutokana na Kagame kuwaweka ndani wale
anaohisi ni wapinzani wake wa kisiasa na wanaotaka kumkwamisha kugombea tena
urais katika uchaguzi mkuu ujao uliopangwa kufanyika mwakani 2017.Waliowekwa
ndani au hata kuuawa katika hali tatanishi ni pamoja na wanasiasa,viongozi wa
kijeshi na watu wenye hamasa kubwa katika jamii wanaoonyesha kupingana nae.
Rais Kagame mwaka jana
aliongoza mabadiliko ya katiba yatakayomwezesha kumpa nafasi ya kugombea tena
urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.Mabadiliko hayo pia yamepunguza muda wa
Rais kukaa madarakani kutokea miaka saba mpaka mitano mabadiliko ambayo
yataanza mwaka 2024 mara baada ya Paul Kagame kumaliza muhula wake wa tatu.
0 comments:
Post a Comment