Mahakama
kuu ya kikatiba ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo jana jumatano imepitisha
maamuzi kuwa iwapo uchaguzi hautofanyika mwezi November mwaka huu basi Rais wa
sasa Joseph Kabila ataendelea kubaki madarakani kwa kipindi kingine zaidi ya muda
wake wa awamu mbili kupita.
Wapinzania
wa Kabila wamepinga uamuzi huo kwa kusema kwamba kama uchaguzi hautofanyika
mwezi November basi atateuliwa mtu mwingine kukaimu nafasi ya urais kwa mpito
hata pale uchaguzi utakapofanyika tena na sio Rais Kabila kuendelea kukalia
kiti hicho.
Kabila
aliekirithi kiti hicho kutoka kwa baba yake alieuawa mwaka 2001 alishinda kiti
hicho kwa kupigiwa kura kwa mara ya kwanza mwaka 2006.Katiba ya nchi hiyo inasema
atatakiwa kuachia madaraka mwezi Desemba mwaka huu baada ya kukikalia kiti
hicho kwa awamu mbili mfululizo lakini serikali inasema uchaguzi huo unaweza
usifanyike kutokana na ufinyu wa bajeti na vifaa vya kuendeshea uchaguzi sababu
zinazoelezwa na wapinzani kuwa ni njama za kabila kutaka kubaki madarakani.
Wapinzania
wanasema Kabila ni lazima atoke madaraka ifikapo mwezi Desember 20 mwaka huu na
kama mahakama inaridhiana na Rais Kabila katika njama zake za kutaka kubaki
madarakani basi watahesabu jambo hilo kama mapinduzi ya kikatiba na
hawatakubali.Wakati wapinzania wakilalamikia jambo hilo la mahakama Ramazani
Shadari katibu mkuu msaidizi wa chama anachoongoza Kabila ameliita tamko la
mahakama kama Ushindi wa wananchi.
Hii
ni moja wa mwendelezo wa viongozi wengi wa Afrika kutafuta namna ya kubaki
madarakani kwa njia yoyote ile.
Moise
Katumbi bosi wa TP Mazembe alietangaza hivi majuzi nia yake ya kugombea Urais
wa nchi hiyo na kuungwa mkono na vyama kadhaa vya upinzani ameingia katika siku
yake ya pili ya mahojiano na serikali juu ya madai ya yeye kupanga njama za
kuiangusha serikali kwa njia za kijeshi kwa kuajiri wapiganaji wakiwemo wanajeshi
wastaafu wa Marekani. Katumbi ambae hapo awali alikuwa rafiki mkubwa wa Rais
Kabila na gavana wa jimbo la Katanga amegeuka kuwa adui nambari moja wa Kabila
hasa kutokana na nguvu aliyo nayo kisiasa na kutishia kubaki madarakani kwa
kabila.
0 comments:
Post a Comment