Katika
kile kinachoonekana ujio mpya wa katibu mkuu wa chama cha Demokaria na
maendeleo CHADEMA ametangaza hadharani nia yake ya kuunda sekretarieti ya chama
hicho na kusema hakuna mbunge hata mmoja atakaepata nafasi.Akieleza kitendo
hicho kama namna ya kuwapa watu wengine wenye ujuzi nafasi za kukiendesha chama
hicho ameeleza kuwa ni jambo la ajabu kwa mtu kupewa nafasi mbili mbili wakati
wapo watu wengi ndani ya chama wenye uwezo wa kuongoza na hawapewi nafasi.
Akiwa
ameambatana na afisa habari wa chama hicho Dr. Mashinji alinukuliwa akisema “Hatuwezi
kuwapa watu kazi mbili mbili,kwanini umpe mtu kazi zaidi ya moja wakati wapo
wengine wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo? Alihoji.
Wajumbe
wa sekretarieti ni pamoja na Katibu mkuu ambae ndiye mwenyekiti, Naibu katibu
mkuu bara, Naibu katibu mkuu Zanzibar, Wakurugenzi wote wa Idara makao makuu,
Wajumbe watano wataalam ambao huteuliwa na mwenyekiti kwa kushirikiana na
katibu mkuu, Katibu wa sekretarieti atakaeteuliwa na katibu mkuu pamoja na
makatibu wa mabaraza ya chama Taifa.
Kwa
sasa mbunge John Mnyika na Grace Tendega huingia katika sekretarieti ya chama
hicho kwa nafasi zao.Swali ni vipi itakuwa hatima yao baada ya maamuzi haya
mapya ya Katibu mkuu.
0 comments:
Post a Comment