Sakata linalomkabili
aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani na ambaye sasa anasaka tiketi ya
kuteuliwa na chama chake cha Democrats kupeperusha bendera ya kugombea Urais wa
nchi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao bi Hilarry Clintoni la kujitengenezea server yake binafsi nyumbani kwake na
kuitumia kupokea na kutuma barua pepe za kiofisi kinyume na utaratibu linazidi
kuchukua sura mpya.
Hillary ambaye FBI
wamepanga kufanya mahojiano naye muda wowote kutokea sasa anakuwa katika wakati
mgumu kujibu ni kwanini alifanya kitendo hicho na kuwa kuna hofu huenda kuna
taarifa za siri nyingi zimevuja kutokana na jambo hilo.
Kufuatia sakata hilo
FBI walianza kufanya mahojiano na wasaidizi mbali mbali wa kiongozi
huyo.Itakumbukwa mwezi April waliohojiana na mmoja wa aliekuwa msaidizi wake wa
karibu bi Huma Abedin na hivi majuzi
aliekuwa msaidizi mkuu wa bi Hilary Clinton kwa muda mrefu bi Cherly Mills alihojiwa mpaka kufikia
hatua ya kuondoka bila taarifa kwa madai kuwa maswali yalivuka mipaka.
Alidai kuwa maswali ya FBI yalivuka mipaka baada ya kutakiwa na FBI aeleze
ni utaratibu gani hutumika katika kutoa barua pepe kwa idara kuu ya mambo ya
nje ya Marekani ili ujumbe ndani yake uweze kutumika kwa umma na Mills ambae ni
mwanasheria kitaaluma alidai kuwa swali hilo hakutakiwa kuulizwa.Hivyo yeye na
mwanasheria wake walitoka nje wakidhaniwa watarudi lakini wakatokomea moja kwa
moja.
Idara kuu ya serikali
ya Marekani inayojihusisha na mambo ya
nje imeshindwa kupata barua pepe yoyote katika server ya bwana Bryan
Pagliano ambae ndiye alikuwa mtaalam wa teknolojia ya mawasiliano na
aliemfungia bi Hilary server yake
binafsi.Pagliano alikataa kujibu swali lolote mwaka jana mpaka Machi mwaka huu
alipokubali kinga kutoka idara ya sheria na kutokea hapo FBI wamekuwa
wakiendelea kumuhoji juu ya sakata hilo na amekuwa akitoa ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment