Soko la wafanya
biashara ndogondogo la Karume wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam leo
limeamka chini ya Ulinzi mkali wa jeshi polisi ili kuzuia wafanyabiashara
waliokuwa wakitandaza biashara zao pembezoni mwa barabara na barabara za akiba (service road) kutofanya hivyo.
Mwandishi wetu
alishuhudia magari mawili yaliyosheheni askari polisi wa kutuliza ghasia
almaarufu kama FFU (Field Force Unity) wakiwa ndani ya magwanda yao ya kazi
sambamba na gari lao la maji ya kuwasha wakijivinjari maeneo hayo.
Tulipata bahati ya
kuongea na mmoja wa waathirika wa kitendo hicho aliejitambulisha kama bwana Baraka
na alipoulizwa aliishia tu kusema “Kaka acha tuisome namba”.
Kwa sasa halmashauri
zote za jiji la Dar es salaam zipo kwenye harakati za kulipanga jiji likae
kwenye utaratibu hasa wafanyabiashara kwa kuwatafutia maeneo japo ni kitendo
ambacho bado kina ukakasi hasa kutokana na kuwataka wahame bila kuwa na sehemu
mahsusi za kuhamia.Tayari meya wa manispaa ya Kinondoni bwana Jacob alishafanya
jambo hili kwa kugawa vizimba pale Ubungo na sasa Ilala baraza la madiwani
halipo kwenye uhusiano mzuri na mkurugenzi wake kutokana na kushinikiza jambo
hili bila kuweka utaratibu bayana kwa wafanyabiashara hawa.
0 comments:
Post a Comment