Balaa laibuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato
unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho.
Taarifa zilizotonywa mtandao huu kutoka kwenye chanzo cha kuamini cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) kilichofanyika juzi Ikulu ya
Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya
chama hicho uliosababishwa na mwenyekiti wao Jakaya Kikwete.
Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya
kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na
mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete
atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli.Taarifa zinasema kabla kilifanyika kikao
kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili
ajenda muhimu ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo.
Mtoa taarifa anaeleza kuwa , kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi
wanne ambao ni Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, Rais Dk. John
Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana ambapo walikubaliana wakatangaze tarehe rasmi, lakini baada
ya kikao cha Kamati Kuu kuanza, Kikwete alikataa kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe,
hatua iliyozua mfarakano.
Yaani ilikuwa hiv,wale viongozi wane walipomaliza kikao chao waliingia
ndani ya kikao cha CC ambacho kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya mkutano mkuu
maalumu ambapo mwenyekiti alirusha na kutaka hoja ya tarehe
isijadiliwe.lipofika ajenda ya tatu ambayo iliwasilishwa na Katibu Mkuu, Kinana
kuhusu kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu,
Kikwete aligoma isijadiliwe na alipoona ananza kuhojiwa kulikoni alifura
kwa hasira na kususia kikao kwa kukiahirisha aliahirisha na kutoka nje.
JK alifatwa nje na kuulizwa kulikoni ndipo alipotoa sababu kuwa mkutano
mkuu ni gharama sana unakadiriwa kugharimu Zaidi ya shilingi Sh bilioni mbili
fedha ambazo anadai hazipo hivyo wajumbe wasubiri zipatikane Kutokana na hali
hiyo yaliibuka makundi mawili, moja linalomuunga mkono Kikwete na jingine
linalopingana na hoja hiyo, likidai kuwa fedha si tatizo kwa chama hicho kwani
kina miradi, ruzuku na marafiki wengi.
Mtoa taarifa anaeleza kuwa ni Jenister Mhagama aliesimama na kumpinga
kikwete hadharan kabla hajakiahirisha kikao akisema suala hilo ni lazima
lijadiliwe kwa kina na tarehe ya mkutano mkuu itangazwe.
“Kauli ya mwenyekiti inaonekana iliwaudhi baadhi ya wajumbe, lakini
Jenista alizungumza vizuri sana na kumhoji mwenyekiti inakuaje hataki kusema
lini utafanyika mkutano mkuu maalumu ili akabidhi chama.
“Maana suala la makabidhiano ni la utamaduni wa ndani ya CCM, Jenista
alisema aliyekaa muda mrefu alikuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pekee
lakini na yeye alikabidhi kwa mzee Mwinyi (Ali Hassan) na pia ilipofika wakati
kama huu mzee Mwinyi naye alikabidhi kwa mzee Mkapa.
“Si hilo tu hata mzee Mkapa naye alikabidhi chama kwake (Jakaya
Kikwete), sasa inakuwaje yeye leo hataki kufuata utaratibu huo ambao ni wa
kawaida ndani ya chama?,” kilihoji chanzo hicho.
Chanzo kingine cha habari kilisema kuwa baada ya mwenyekiti huyo wa CCM
taifa kuahirisha kikao hicho juzi, aliondoka na kurejea jijini Dar es Salaam
kwa gari tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa.
“Ratiba ya chama ilikuwa baada ya kikao cha jana (juzi) mwenyekiti
angelala Dodoma na badala yake alipoahirisha kikao kwa utata alipanda kwenye
gari na kuondoa hali ya kuwa alitakiwa kurejea Dar leo (jana).
“Baada ya kikao hicho alitoka mzee Kinana akiwa amekasirika sana, tena
huku akiwa amekunja sura, unajua siku zote mzee Kinana anaamini kwamba kile
kilichokuwa kinapiganiwa na chama hivi sasa ndicho kinachotekelezwa na Rais
Magufuli tena kwa vitendo tofauti na huko nyuma,” kilisema chanzo chetu.
0 comments:
Post a Comment