Kati
ya majina ya utani ambayo Donald Trump mgombea wa kiti cha urais wa Marekani
kwa tiketi ya chama cha Republican basi ni “The Beast” yaani
Mnyama. Hii ni kwa sababu ameweza kuwafurusha wapinzani wake wote ndani ya chama
chake kujitoa hivyo kujihakikishia kuipeperusha bendera ya chama hicho kwenye
uchaguzi unaotarajiwa.
Usiku
wa jana wana Republican walishuhudia mgombea wao mwengine John Kasich akijitoa
kwenye mbio hizo pale Columbus, Ohio. Kasich mgombea pekee aliekuwa amesalia
akiminyana na Trump alihitimisha harakati hizo kwa kutoa tamko lililogusa hisia
za watu wengi. Alinukuliwa akisema “Nimekuwa
siku zote nikisema Mungu ana makusudi na mimi kama alivyo na makusudi na kila
mmoja wetu. Na kama ninavyohitimisha kampeni zangu leo, nina imani mpya
kabisa,imani kuu kuwa Mungu atanionyesha kusudio langu na kunifungulia njia
mpya”. Baada ya hapo aliwashukuru wote waliojitoa kwa hali na mali kwa ajili
ya kumsapoti na kueleza furaha aliyo nayo kwa kuwania nafasi ya ofisi ya juu
kabisa katika taifa.
Wakati huo huo sasa ni
Dhahiri kuwa Donald Trump anajipanga kuhakikisha Bernie Sanders hapitishwi na
chama chake badala yake anamuhitaji Hillary Clintoni akidai huyo ndio
atammaliza asubuhi na mapema kuliko Bernie.
0 comments:
Post a Comment