Haya
sasa ndio maendeleo yanayohitajika Afrika kwa wakati huu.Zipline kampuni ya kutengeneza “maroboti”
inafanya kazi na serikali ya Rwanda kuwatengenezea drones zitakazotumika kusambazia vifaa tiba kwa haraka na wepesi
zaidi kwa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.Ubunifu huu utakuwa wa kwanza na wa
aina yake kwa bara la Afrika.
Namna
zitakavyofanya kazi ni kuwa madaktari na wauguzi katika maeneo yao watakuwa
wakiweka maombi kwa njia ya simu na drones zitakuwa zikichukua vifaa hivyo
kutoka kwenye maghala maalum yaliyotengwa sehemu mbalimbali za nchi na
kuzipeleka eneo husika ndani ya dakika chache tu na zikifika vifaa vitashushwa
kwa parachuti.
Drones
hizo zitakuwa zikitumia betri na zina uwezo wa kubeba kilo 1.5 na uwezo wa
kusafiri mpaka kilomita 120.Ubunifu huo utaanza kutumika mwezi July kwa
kusambaza damu nchi nzima.Matumizi haya ya drones yatapunguza muda wa
usambazaji vifaa hivi kutoka kutumia masaa 15 sasa havitachukua hata dakika 15.
Akiliongelea
suala hili mwanzilishi na Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Zipline mwenye umri
wa miaka 29 Bw. Keller Rinaudo amesema wazo hili alilipata kwa mara ya kwanza
mwaka 2014 alipotembelea Tanzania na kugundua kuwa kunahitajika njia ya haraka
ya kusambaza vifaa tiba sehemu za vijijini.Amesema Rwanda ndio wa kwanza
kununua wazo hilo lakini ana mpango wa kulisambaza kote Afrika.
0 comments:
Post a Comment