Wanasayansi wa Uchina wamefaulu katika tiba yao mpya ya majaribio ya
kutibu upofu na imeonekana kufanikiwa sana.
Walitumia nguruwe
katika majaribio hayo ya tiba ya kuondoa upofu, ambapo walitumia konea kutoka
kwa wanyama hao.Mtu wa kwanza kupata tiba hiyo ni kijana Huang Yuanzhen kutoka Jiangxi China. Madaktari kutoka Chuo
cha Zhongshan huko Guangzhou wamesema hii ni tiba mujarabu na rahisi
sana kupatikana.
Sasa wamesema wana
imani kwamba hilo litafaa sana kutokana na uhaba wa konea za binadamu.Inakisiwa
kuwa Wachina wapatao 5 milioni wanakabiliwa na matatizo ya konea, sehemu ya
mbele ya jicho iliyo ngumu na inayowezesha miali ya mwanga kupenya.Lakini ni
konea 5,000 pekee ambazo hupatikana kila mwaka.
Matatizo ya konea
husababisha watu wengi kuwa kipofu.Njia hiyo mpya ya kutibu upofu imeanza
kutumiwa baada ya kuidhinishwa na serikali mwaka jana.
Konea kutoka kwa
nguruwe hutibiwa na kutolewa bakteria na virusi, pamoja na kutolewa DNA ya
nguruwe, kabla ya kupandikizwa katika jicho la mwanadamu.Wakosoaji wa mpango
huo wanasema Uchina inaenda kwa kasi sana, bila kuangazia madhara ya mpango huo
kwa kipindi kirefu.
0 comments:
Post a Comment