Papa Francis anategemewa kukutana na kiongozi mkuu wa madhehebu ya sunni duniani Shekhe Ahmed al-Tayeb mjini Vatican Jumatatu.Kiongozi huyu mkuu na Imam wa msikiti mkubwa na wakipekee wa madhehebu ya suni uliopo Cairo Misri Al-Azhar atakuwa na hadhara na papa Francis katika basilika la Mt.Petro mjini Vatican.
Mashirikiano kati ya hizi imani mbili yaliingia
ukakasi katika uongozi wa papa Benedict wa kumi na sita baada ya mwaka 2006
kutoa kauli zilizochukuliwa kama za kuutangaza uislam kama dini ya
vurugu.Mazungumzo yalianza tena mwaka 2009 lakini yalisimamishwa tena na
Al-Tayeb mwaka 2011 baada ya papa Benedict kuomba wakristo wachache
waliolipukiwa na bomu katika kanisa la Alexandria walindwe.
0 comments:
Post a Comment