Figisu Zaendelea DRC: Moise Katumbi Afunguliwa Mashtaka Ya Kutaka Kumdhuru Rais Kabila


Moise Katumbi,mwanasiasa na mfanyabiashara alietangaza nia yake ya kugombea urais wa Jamuhuri ya watu wa Congo sasa atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuajiri wapiganaji wa kimarekani kwa lengo la kumdhuru Rais kabila,msemaji wa serikali Lembert Mende amesema.
Rais Kabila ambae yupo katika kipindi chake cha mwisho cha uongozi kikatiba amekuwa akionekana kama mtu asiyetaka kuachia madaraka hayo hasa baada ya Mahakam kuu ya nchi hiyo kutoa maamuzi kuwa anaweza kubaki katika nafasi hiyo ikiwa uchaguzi hautafanyika mwezi November.Serikali nayo imekuwa ikitoa visingizio kedekede ili kutofanikisha uchaguzi huo.
 
Katumbi,mtu ambae hapo awali alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Kabila ghafla amegeuka adui yake nambari moja hasa baada ya kutangaza nia yake ya dhati ya kutaka kurithi kiti cha urais.Sasa kumekuwa na kila aina ya figisufigisu kuhakikisha hagombei nafasi hiyo.
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment