MWIGIZAJI
wa filamu na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba
hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa
mwili wake.
Hemed anayetamba na wimbo wake wa ‘Imebaki stori’, alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni poda, lipshine na pafyum na hataacha kujiremba.
“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama poda na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni staa natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.
“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemed.

0 comments:
Post a Comment