Bao la Eden Hazard la dakika ya 83, litakuwa bao la historia katika klabu ya Leicester City. Likiwa ni bao la kusawazisha la Chelsea na kufanya matokeo kuwa 2 - 2 dhidi ya Totenham.
Goli hili limefuta kabisa ndoto za Totenham kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu huu. Totenham walitangulia kufunga dakika ya 35 na 43 kwa magoli yaliyofungwa na H.Kane na H.Son.

Leicester wanaandika rekodi ya kipekee na hii ikiwa ni mara yao ya kwanza kutwaa taji hilo. Ikumbukwe kuwa msimu ulioisha Leicester City walikuwa wakigombea nafasi ya kutokushuka daraja.
0 comments:
Post a Comment