“The Strain’’ hii ni bonge la tamthilia
linaloonyesha jinsi kitengo cha kupambana na kuzuia magonjwa kilivyoitwa uwanja
wa ndege wa JFK kuchunguza chanzo cha
vifo vya abiria 200 waliokuwa kwenye ndege. Kitengo kinagundua kuwa kuna
mlipuko wa virusi ambao baada ya muda mchache na kwa sababu vinasambaa kwa kasi
watu wote watageuka vempire na kuutokomeza kabisa ubinadamu. Hatari Zaidi
virusi hivi vimetengenezwa na mwanadamu katika ubinafsi wake wa kutaka utajiri
na mali.
Daktari Goodwether na wenzake ndio
wanashikilia hatma ya ubinadamu mikononi mwao kwa kuamua kupambana na virusi
hivi. Ni tamthilia ya kutisha na kusisimua sana na itakufanya usibanduke
ukianza kuitazama. Tamthilia hii itakufikirisha Zaidi kama kweli virusi vya
UKIMWI ama EBOLA ni janga la asili ama ni husda za mwanadamu katika kutafuta
ukuu.

Season 1 na 2 zote zimetoka na zimekamilika zikiwa na jumla ya episodes 26 (13 kwa kila season) ilianza kurushwa tarehe 13, July 2014 na epsode ya 26 ilirushwa 4, October 2015. Kuhusu Season 3 Tayari wameshaanza kushoot japo bado hawajatangaza tarehe rasmi ya kushusha mzigo huo.
0 comments:
Post a Comment