Umewahi kusikia
visiwa vinavyoitwa British Virgin Islands? Utastaajabu kuwa huu ni mkusanyiko wa
visiwa vingi vidogo vidogo sana lakini vikuu vikiwa ni Tortola ambapo ndipo
kuna mji mkuu wa visiwa hivi,Virgin Goda, Jost Van Dyre na Anegada. Visiwa hivi
viko chini ya utawala wa Malkia Elizabeth wa Uingereza lakini wakiwa na waziri
wao mkuu anaeitwa Dr. D. Orlando Smith na gavana wao John S. Duncan
Kwa sensa ya
mwaka 2015 mwishoni ilionyesha jumla ya raia katika visiwa hivi ni watu33,454
yani kama ingekuwa ni Tanzania basi idadi hii ni sawa ama ndogo ukilinganisha
na idadi ya wakazi wa mtaa wa Kariakoo.Japo ipo chini ya milki ya waingereza
lakini asilimia 82 ya raia wake ni watu weusi wakati weupe kabisa kwa maana ya
waingereza halisi ni asilimia 6.8 na waliobaki ni mchanganyiko.
Ajabu lingine ni
kwamba visiwa viko chini ya milki ya waingereza lakini sarafu wanaotumia ni
dola ya kimarekani hii ni kutokana na ukaribu wa kiasili uliopo kati ya visiwa
hivi na vile vya US Virgin Islands hivyo hata tamaduni nyingi zimeshibana.
Shughuli kuu inayoingizia kipato visiwa hivi ni Utalii ukifuatiwa na shughuli
za kifedha.Mfano, inakadiriwa kuwa watalii zaidi ya milioni moja hutembelea
visiwa hivi kwa mwaka.
Visiwa hivi
miaka ya kuishi ya binadamu ni wastani wa miaka 78 na ni moja ya sehem nzuri
duniani kuishi na kufurahi. Pamoja na vile visiwa vya US Virgin Islands huitwa
pepo ya duniani. Huku hakuna magonjwa ya kuambukiza wala shida uzisikiazo
mataifa mengine, Huku ni kuishi tu mpaka Mungu atakapoamua kukuchukua (Kwa
wanaoamini Mungu)
Chaka la kimataifa la makampuni hewa kufichia na
kutakatishia fedha
Moja ya sifa
kubwa na inayosumbua akili za watu sasa hivi ni hii ya visiwa hivi kutumika
kama kichaka cha matajiri,viongozi wa umma na makampuni binafsi pamoja na watu
maarufu kufichia fedha zao ama kufungualia makampui hewa.Zipo skendo nyingi
sana zinazohusiana na kichaka hiki. Hata wakati fulani uchumi wa dunia huyumba
kutokana na shughuli zinazoendelea visiwani humu vya utakatishaji fedha “Money laundering”.
Imebainika kuwa
sio watu binafsi tu hata viongozi wakubwa wa dunia wanahusika katika skendo
mbali mbali zinazohusiana na utakatishaji fedha. Hata serikali baadhi za dunia
hufikia kuwezesha zoezi hili na hivyo kufanya biashara hii haramu kuwa ngumu
kudhibitika.
Kwanini watu
hufungua makampuni hewa na akaunti za benki visiwani humu?.Ni kwasababu hakuna
kodi ya aina yoyote ile inayolipwa na hivyo wataalam wanapaita “ a place of classic tax heaven”. Huku
mapato yake hutokana na kodi za wafanyakazi katika mishahara yao na kodi ya ardhi
kwa wakazi ambapo wengi wao ni mawakala wa utakatishaji fedha.
Tabia hii ilianza
mwaka 1980 pale ilipopitishwa sheria ya kuruhusu wageni kufungua makampuni na
akaunti za benki visiwani humo bure na mwaka 1994 ikapitishwa sheria ya usiri
na ufaragha. Mambo hayo mawili yalipelekea mpaka kufikia mwaka jana kuna
makampuni hewa na akaunti za benki zaidi ya 400,000 ambazo siyo za wakazi wa
visiwa hivyo.Sheria ya usiri inasababisha hakuna taarifa yoyote unayoweza
kupata juu ya akaunti yoyote ukapewa zaidi ya mmiliki tu.
Moja ya skendo
kubwa kuwahi kutokea ni ile iliyovumbuliwa na kundi la waandishi wa habari wa
kimarekani wa Internatinal Consortium of Investgative Journalists (ICIJ)
wakisaidiana na waandishi wengine 80 kutoka nchi 46 duniani. Waandishi hawa
walifanikiwa kupata “hard drive” ya
kompyuta yenye ukubwa wa 260 GB iliyokuwa na mafaili zaidi ya milioni 2.5
kutoka mataifa makubwa 10. Mafaili hayo yalihusisha kampuni zaidi ya 122,000 na
taarifa za watu 130,000 ambao ni wamiliki, ama wawezeshaji ama mawakala wa
makampuni feki ama wamiliki wa akaunti za fedha huko. Idadi kubwa wakiwa ni
kutoka China, Hong Kong, Taiwan, Singapore na Urusi.
Skendo hiyo
maarufu kama Panama papers
ikiwahusisha marais kama Putin wa Urusi ambapo taarifa zinaonyesha washirika
wake ama yeye mwenyewe wakimiliki zaidi ya dola za kimarekani bilioni 2, Rais
wa China Xi Jinping, Raisi wa Ukrane Petro Poroshenko, baba wa waziri mkuuwa
sasa wa uingereza David Cameroon na mlolongo mrefu wa
marais mawaziri wakuu wafanyabiashara na watu maarufu.
Alipokuwa
akijibu sakata hili waziri mkuu wa visiwa hivyo kwa kiburi kabisa alisema (Kwa
tafsiri isiyo ya moja kwa moja) “Tunawahakikishia wateja na wadau wetu wa
Hong Kong na kote duniani kuwa hili tukio la kuvuja kwa taarifa ni la bahati
mbaya. Bado tunajiamini na tutaendelea kuwatunzia siri zenu kwa ufaragha
mkubwa”
Itakumbuka hata
hapa Tanzania kwenye sakata la IPTL na Tegeta Escrow visiwa hivi havikuwa mbali
katika uhusika wake.
Tatizo kubwa
limekuwa ni sheria ya usiri katika taarifa za kifedha ndani ya visiwa hivi.
Uingereza ina uwezo wa kuifuta sheria hii na hivyo kuleta uwazi katika sekta ya
kifedha “financial transiparency”
lakini haitaki kufanya hivyo.Swali ni kwanini?
Ni kwa vipi BVI ilitokea kuwa chaka la usiri mkuu
namna hii? Kwanini imeshindikana kutoa sheria hii ya usiri?
Nani yupo nyuma ya visiwa hivi?
0 comments:
Post a Comment