Leo tujikumbushe skendo iliyolitikisa
taifa la Marekani hasa familia ya Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton ya
kuhusiana kimapenzi na mfanyakazi wa Ikulu bi Monica Lewinsky.Wengi tumesahau
lakini ni moja ya skendo zinazosisimua sana kuzisoma.Leo tutaipitia japo kwa
juu juu na kwa lugha nyepesi ya kiswahili
Ilianzaje?
Ilikuwa ni mwaka 1995 wakati huo Bill
Clintoni akiwa katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi marekani akiwa na umri
wa miaka 46.Monica yeye alianza kufanya kazi Ikulu katika ofisi ya katibu mkuu
kiongozi (Chief of Staff) Leon Paneth tangu June, 1995 kama mfanya kazi
mwanafunzi (Intern) akiwa ametoka kuhitimu chuo cha Lewis & Clark
college.Ni hapo Bill Clinton alipomuona na kuvutiwa na binti huyo aliekuwa bado
mchanga na mbichi wa miaka 21 tu na kwa mujibu wa Monica walianza mahusiano na
Rais November mwaka huohuo.
Ilikuwaje?
Baada ya Rais kuwa na mahaba na
Monica na hivyo kunogewa nayo msaidizi wa katibu mkuu kiongozi bi Evelyn
Liberman alishtukia mchezo na April 1996 aliamua kumwamisha Monica katika ofisi
ya msemaji msaidizi wa wizara ya Ulinzi (Pentagon) bwana Ken Bacon.Bi Evelyn
alitoa sababu kuwa amemwamisha kutokana na Monica kuonyesha tabia zisizofaa na
za kitoto “inappropriate and immature
behavior".Lakini pia watendaji wengine walikuwa wakitilia shaka ukaribu
uliopitiliza kati ya Monica na Rais. Ni katika ofisi hiyo za pentagon ndipo
Monica akakutana na Linda Tripp binti aliyekuwa mfanyakazi wa idara ya Ulinzi
katika wizara hiyo wakaunda urafiki.
Kutokana na ukaribu wa kiutendaji
kati ya Pentagon na Ikulu bado Monica alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa anafika
Ikulu mara kwa mara na mara zote alitumia muda mwingi sana katika ofisi ya Rais
kitu ambacho bado hakikuwa kikiwafurahisha wafanyakazi wa Ikulu na hivyo
October 1997 Ikulu iliandaa mpango wa
kumwamisha tena bi Monica na kumtaka ahamie ofisi za umoja wa mataifa UN. Ni
balozi Bill Richardson alieombwa ampangie kazi Monica lakini baada ya usaili wa
kazi bi Monica aliikata nafasi hiyo na hivyo kubakishwa Pentagon.
Ikumbukwe mpaka wakati huo hakuna
aliekuwa na ushahidi pasi shaka kuwa Monica ana “date” na Rais Clinton.Ni mwaka
huo hasa baada ya kuona anazidi kuwekewa vipingamizi vingi vya kukutana na Rais
mara kwa mara ndipo alipoanza kumueleza Linda Tripp rafiki yake wa wizara ya
ulinzi juu ya mahusiano yake na Rais.Alimweleza kuwa kati ya November 1995
mpaka March 1997 alishakutana kimwili na Rais Clinton mara tisa.Linda baada ya
kusikia hivyo aliwasiliana na mwanausalama Agent Lucianne Goldberg aliempa
kifaa cha kurekodia simu na hivyo Linda akamtegeshea Monica na kurekodi simu
zote alizokuwa akiwasiliana na Rais Clinton.Ni katika kipindi hicho pia kuna
siku Linda Tripp alikutana ana Monica akiwa anatoka kwenye ofisi ya Rais nywele
zikiwa zimemvurugika na rangi ya mdomoni ikiwa imebanduka.
Skendo iliibukaje?
Baada ya Monica kugoma kutoka
Pentagon lilitoka shinikizo kutoka Ikulu na haraka aligundua anafukuzwa kazi
hivyo aliamua kuacha kazi kwa kuahidiwa na Rais kuwa atamtafutia kazi nyingine.
Rais Clinton kwa kumtumia msaidizi wake Betty Curie aliyekuwa akijua
kinachoendelea kati ya Rais na Monica aliamua kumtumia rafiki wa karibu wa
Clinton bwana Vernon Jordan amtafutie kazi Monica.
Sasa baada ya Linda Tripp kukamilisha
kukusanya ushahidi wake agent Goldberg alimwelekeza Linda apeleke mkanda huo
kwa mwanasheria wa kujitegema Kenneth Starr aliyekuwa akichunguza skendo
nyingine za Clinton kama ile ya Whitewater
,White House FBI filter Controversy
na ile ya White House Travel office
controversy .Baada ya kumfikishia Kenneth
yeye sasa angepeleka kwa Paula Jones(Kuna sababu maalum ya kufanya
hivi).
Mkanda ulipomfikia Paula Jones alimwita
Monica na kumwambia madai hayo Monica alikataa na ndipo hapo walipowasiliana na
mwandishi wa habari Michael Isikoff wa gazeti la Newsweek. Mnamo Januari 17 ,1998 Michael katika Drudge report alipoamua kuirusha hiyo habari kwa mara ya kwanza.
January 21, 1998 gazeti kubwa la Washngton Post nalo likaruka na hiyo skendo na
ikaanza kuwa kubwa na isiyo mithilika.
Kwa mara ya kwanza January 26, 1998
Rais Clinton akiwa anaongea na waandishi wa habari Ikulu akiwa sambamba na
mkewe bi Hilarry alikataa katakata kujihusisha kimapenzi na Monica. Hata
alipoletewa rekodi za maongezi yao Rais alikataa na kuondoka haraka kwa kudai
kuwa anaharaka ya kwenda kuandaa spichi ya kuwasilisha hali ya uchumi ya Taifa.
Nini Kilifuata baadae?
Habari ni ndefu ila itoshe tu kusema
baada ya hapo yapo mengi sana yaligundulika na kuendelea na kulitokea msukumo
kuwa Rais ajiuzulu na yeye Februari 6,1998
akajibu “Kwa imani watu wa nchi hii waliyonipa kwa kunichagua kuwa Rais
wao kamwe siwezi waacha kwa sababu hii”. Hilary clinton mkewe nae aliamua
kuziba masikio na February 11, 1998 alinukuliwa akisema “Suala hili si zito
sana litakwisha tu” .
Skendo hii ni ndefu saga litaendelea.
0 comments:
Post a Comment