Katika vitu
amabavyo Gadner Habash anaweza akawa anajutia kwa sasa basi ni kitendo cha
kutoa kauli iliyoonekana kumdhalilisha aliyewahi kuwa mke wake kwa zaidi ya
miaka kumi na tano bibiye Judith Wambura Mbibo almaarufu kama Lady Jaydee
Komando.
Kauli hiyo
aliyoitoa hivi majuzi kwenye tukio moja la starehe limekera watu wengi sio
wanaume wenzake tu bali hata wanawake wanaoona kudhalilishwa kwa mwanamke
mwezao kwa kauli ile.Akiongea kwa hasira na masikitiko makubwa Mkurugenzi mmoja
wa biashara na masoko katika moja ya kampuni kubwa sana hapa nchini alinukuliwa
akisema “Labda nife ama nitoke kwenye hii nafasi lakini kamwe Gadnera hatakaa
apate tangazo letu kwenye kipindi chake,nasema kamwe”
Nae Meneja wa
masoko wa kampuni moja ya mawasiliano ya simu za mkononi alisema “Ule ni ujinga
sasa siwezi peleka tangazo kwa mtu kama yule. Afute kabisa akilini kuniona
kwake’”.Bado kumekuwa na mkanganyiko wa kama alikuwa sahihi kusema maneno yale
ama la. Vyanzo vya ndani vya watu wa karibu na Gadner vinasema mwenyewe anajutia
kauli ile na kuwa siku yoyote akiwa tayari ataomba umma wa wa Tanzania radhi.
Ikumbukwe
kampuni zote hizi zilikuwa na matangazo naye na deals nyingine nyingi za zaidi ya milioni 100.
0 comments:
Post a Comment