Mengi
yameandikwa tangu hii issue ya PANAMA papers ivamie mitandao jana.Wengi
wamechambua na kuanika majina yanayohusika na ishu hiyo lakini mtandao huu kama
kawaida yake utakupeleka one step ahead.Jana
(Jumatatu) tuliahidi kukuletea exclusively
watu waliohusika na kutajwa katika skendo hii matata ya PANAMA papers.Kufuatia
maoni ya wengi ya kutaka kujua baadhi ya mambo kwa kina zaidi tuliridhia kuwa
tunahitaji kuchimba zaidi na hivyo kuja na kitu deep.Bado wachimbaji wetu wanaendelea na wakimaliza utapata kujua
ambayo hakika huyajui.Utapata kujua jinsi gani wakati sisi tukiishia kwenda
Mabibo na Kinondoni manyanya kuna watu wanafanya biashara na wako dunia ingine
tofauti kabisa lakini viwiliwili vyao vikiwa Tanzania.Utapata kujua jinsi gani viongozi
wetu wa serikali za dunia na wafanyabiashara zilivyo na mtandao
usiomithilika.Hapahapa tiadventurers.blogspot.com
Lakini
leo tusikuache hivi hivi kuna mambo kidogo yaanze kukushangaza.Katika
kalabrasha la PANAMA kuna kampuni tatu zimetajwa kuhusishwa na Tanzania
Wheelock Holding ltd, Richmond Finance Corporation na Expro Energy Ltd.Hii ya
mwisho imesajiliwa juzi tu mwaka 2014.Sasa hii kampuni ndio tutakayodili nayo
kwenye makala zijazo.
Kalabrasha linaitaja kampuni ya SUN MINING COMPANY LTD kama mmoja wa maafisa wanaohusishwa na hili saga.Hii kampuni utapata ifahamu kiundani ila inshort inapiga mzigo hapa Tanzania kenya na Mali.Inajihusisha na uchimbaji wa madini ya Iron,Manganese,Copper na Chrome ikiongozwa na bwana Ashkin Akbar.Unajua kodi iliyokwepa mpaka sasa?Unajua mabalaa yake mengine.Basi subiri.
Halafu
taarifa zinaonyesha tena katika hilo kalabrasha kuwa kuna maofisa 53 watu wa
kati 3 na adresi 38 zinazohusishwa na zipo Tanzania.Sasa tusirudie kuandika
kitu ambacho tayari unaweza kisoma, kama bado hujalisoma hilo kalabrasha fungua hapa https://offshoreleaks.icij.org/#_ga=1.72650774.467971681.1462812105
Sasa,kwenye
kalabrasha utaona idadi kubwa ya wahindi/waarabu ama watu wa jamii ya kiasia
karibu asilimia 95 ya maofisa waliotajwa huko halafu utamuona jamaa mmoja MKURYA anaitwa Konsel James Wambura ambae anahusishwa na kampuni ya Funsway
Holding Ltd iliyosajiliwa Samoa yenye makazi China.Yani wakati kukiwa na notion kuwa wachaga ndio wapiga dili
hapa mjini sasa kuna wakurya waliovuka borders.Huyu
bwana ni nani?ana shughuli gani?kashapata dili gani za serikali?Hayo maswali
yote ndiyo yatajibiwa makala itakapokuwa tayari.
Halafu
tena utaona kuna watu wenye asili ya kiasia kama ilivyokwisha tamkwa hapo juu kati
ya hao watu, watu watano wanahusika kwa karibu sana yani pigia mstari kwa
karibu sana na mijamaa inayomsumbua Rais katika suala la sukari.Taarifa zao
kamili na uhusika wao hakika utaupata hapahapa.
Sasa
kama ulikosa kusoma makala iliyoandikwa “BRITISH
VIRGIN ISLAND: Chaka la makampuni hewa,kufichia na kutakatishia fedha”
itafute kwenye feed ya Habari za Uchumi hapahapa.Itakusaidia kuelewa mambo
kabla ya kufunuliwa la PANAMA papers.
0 comments:
Post a Comment