Maisha, Mungu Na Kifo....Ukweli Halisi – Sehemu I


 
 
Na: Bounavista

 
Miaka zaidi ya 10 iliyopita nikiwa darasani mwalimu alitoa mfano "umepanda basi..baada ya safari ndefu kidogo basi likakwama, unatakiwa kusaidia kulisukuma.ila unatakiwa kulisukuma ukiwa ndani ya basi" alimalizia, ni dhahiri kwa mfano huu ..kila mtu alicheka na kumuona mwalimu amewehuka..utasukumaje basi ili hali ukiwa ndani? mwalimu alitoa mfano huu baada ya mimi kumuuliza kwanini tupo duniani? sisi ni nani?,nilimuuliza haya maswali nikiamini kwakua ni mwalimu..basi anajua mengi.sikutambua ila mwalimu kwa kuona uzito wa kujibu maswali haya aliamua kujibu kwa mfano..alifananisha maisha na basi..na sisi kama abiria...kujaribu kutambua siri za maisha haiwezekani.
 
 
Ni miaka zaidi ya 10 imepita ...sasa nagundua mwalimu alikua sahihi katika jambo moja..kutambua hasa siri za dunia hii..ni lazima utoke nje zaidi ya wewe ulivyo,kwa kupitia safu hii ...nitakuletea ujumbe wa kweli kabisa kuhusu siri za dunia hii...UJUMBE WA KWELI KABISA nilioupata baada ya kuelezwa na walioko pema ..waliotangulia,utakua sahihi kabisa endapo wakati unasoma makala hii unawaza ni kwa vipi nimepewa ujumbe huu,kabla ya kueleza kwa ufupi nitatoa angalizo.
 
Taarifa zinazotolewa kwenye makala hii..ni taarifa zenye ukweli kwa 99% ,zinaweza kuleta mfarakano wa kimawazo kati ya dini yako na wewe.
 
Ninachoeleza hapa..ni sawa kabisa na expirience (pito) alilopitia Yohane(ufunuo 1:10)..alieandika kitabu cha ufunuo kinachopatikana kwenye bibilia...naandika kuhusu taarifa/ujumbe uliopatikana baada ya kutoka nje ya huu mwili (astral body) na kuwasiliana na wanadamu ambao hawana mwili tena..ila wako kwenye ngazi ya juu kabisa ya utakatifu. Hawa hujaribu kuwasiliana na baadhi ya wanadamu kwa njia mbalimbali lengo likiwa kusaidia na kuokoa..ifahamike kua si kila mtu anaweza ku BAHATIKA kuwasiliana nao. Napenda kutoa angalizo kuhusu kitendo cha kujitoa nje ya mwili..sio salama kama inavyoaminika na watu wengi..na SIO lengo la makala hii kuelimisha jinsi ya kujitoa nje ya mwili (astral projection) bali kuleta na kushirikishana ujumbe na siri mbalimbali za dunia hii na baada ya kifo kwa lengo la kusaidia wale ambao hawatambui bado..na kuwapa nguvu wale ambao bado wako safarini.Lengo la makala hii ni kuleta ufahamu zaidi na uelewa juu ya baadhi ya mambo ambayo yanaandikwa au mengine mengi ambayo yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku.Lengo ni kuleta UHURU KAMILI.kutoka nje ya mwili ni njia pekee iliyokua inatumika,inayotumika na pengine itakayoendelea kutumia kuwasiliana na viumbe wengine nje ya ngazi hii tunayoishi..ni nani unawasiliana nae baada ya kutoka nje ya mwili..hii ni juu ya muhusika na hapa ndipo hatari ipo.
 
Makala hii ndio imeanza na itaendelea hapahapa.....

 
Share on Google+

About TANZANIA INVESTEMENT ADVENTURERS

We are an Investment Club geared to use social networks as means of sharing informations, knowledge, wisdom but more importantly reducing the cost of marketing your products by reaching so many potential customers with the lowest cost ever.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment