Loh,
huwezi amini yaani kumbe vita yote ile ya meno ya tembo tukijua hilo limtu lipo
sayari gani sijui kumbe tunaishi nalo hapa hapa. Ni bibi Yang
Fenglan mwanamke wa kichina alieingia
Tanzania mwaka 1970 na ni mchina wa kwanza kuhitimu masomo ya kiswahili na
hivyo kuajiriwa na TAZARA kama mtafsiri ndiye hasa anaeshikilia biashara haramu
ya meno ya Tembo Duniani kutokea Tanzania.
Bibi huyu inakadiriwa tangu mwaka 2000 mpaka 2014
ameshafanikiwa kuua zaidi ya tembo 400 na hivyo kusafirisha zaidi ya pembe 700
zenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano. Bibi huyu amekana
mashtaka na kesi yake imepangwa kusikilizwa tena mwishoni mwa mwezi huu.
Yang
Fenglan ni nani?
Yang Fenglan bibi wa miaka 66 mchina mwenye ujuzi wa
kuongea kiswahili zaidi ya mzaramo alikuja Tanzania mara ya kwanza mwaka 1970
na baada ya kufanya kazi TAZARA mwaka 1975 alirudi zake china kufanya kazi na
idara ya biashara za kigeni ya Beijing. Ni mwaka 1998 alipoamua kurudi Tanzania
kufungua biashara, kwa mwendo huu tutasema alifungua biashara zaidi ya
moja (na hii ya meno ya tembo)
Alikodi stoo mbili hapa Dar es salaam na akafungua
mgahawa wa kichina ghorofa ya chini na juu akafungua kampuni ya uwekezaji
akaiita Beijing Great Wall Investment. Mgahawa ulifanikiwa sana lakini mwaka
2014 yeye mwenyewe alisema “Sasa hivi siutegemei mgahawa katika kuniletea pesa
badala yake nautumia kama sehemu ambayo wachina na watanzania wanaweza kukutana
na kubadilishana mawazo”
Mwaka 2012 alikuwa ni katibu mkuu wa baraza la biashara
kati ya Tanzania na China na aliwahi nukuliwa akisema “Najua sasa hivi
ningetakiwa niwe nimestaafu lakini ujuzi wangu wa lugha na mtandao nilionao
unaweza wasaidia watanzania na wachina wengi kujuana na kuaminiana
kibiashara.Sitaki kuachia nafasi hii.Mimi ni mfano halisi wa mahusiano kati ya
China na Tanzania”
Kukamatwa kwa bibi huyu kumepokelewa kwa furaha kuu na
wadau wa wanyapori na kusema sasa tatizo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa
kwani karibu wachina wote wanaokamatwa na pembe za ndovu nchi hii kama
hawakutumwa na yeye basi waliowatumia wana mahusiano na mama huyu. Hivyo bibi
huyu huitwa “Queen of Ivory”
0 comments:
Post a Comment