Donald Trump mgombea wa
kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amesema yupo
tayari na angependa kuzungumza na kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un.
Trump ameseam angependa
kuongea nae ili amwambie aacha majaribio yake ya Nyuklia.Amenukuliwa akisema “Ningependa
kuongea nae,Sina tatizo katika kuongea nae na jambo kubwa nitamwambia aache
majaribio yake ya ki nyuklia” alisema.Aliongeza kuwa “Nitaongeza jitihada pia
kuwaambia China waiambie Korea Kaskazini iache majaribio hayo,sisi bado tuna
nguvu kubwa dhidi ya China” aliongeza.
China ni miongoni mwa nchi
chache ambazo zinajihusisha na kuwa na uhusiano mzuri na Korea
Kaskazini.Utawala wa Obama ulijitahidi kuwasukuma China waikanye Korea
Kaskazini lakini ulishindwa na Marekani haikuweza kuifanya lolote China kwa
kuogopa madhara ambayo yangeweza kutokea.
0 comments:
Post a Comment