Rais wa Venezuela Nicolaus Maduro ameishutumu Marekani kwa madai ya
kufanya njama ya kutaka kuipindua nchi yake.
Rais huyo pia
ameishutumu Marekani kwa madai ya kupanda mbegu ya machafuko katika nchi hiyo.Anasema
Machafuko hayo wanataka kuyaumia kupotosha watu ili waone serikali yake haifai
hivyo wananchi waamue kumtoa madarakani.Ameishutumu Marekani kwa kurusha ndege
zake katika anga la Venezuela mara mbili bila kupewa ruhusa.Hali hiyo
ilimpelekea Rais Nicolas Kutangaza hali ya hatari nchi Venezuela.
Wakati huo huo
Kiongozi wa upinzani nchi humo Henrique Capriles amelitaka jeshi la nchi hiyo
kuchagua kumtii Rais Maduro au kuitii katiba akimshutumu rais huyo kwa
kutangaza hali hatari wiki iliyopita.
Capriles amemshutu
bwana Maduro kwa kutangaza hali ya tahadhari nchini humo wiki iliyopita. Kabla
ya bunge la nchi hiyo kupinga uamuzi huo wa rais, Maduro alisema agizo hilo
lilihitajika kwa sababu uhuru wa taifa hilo ulikuwa unakabiliwa na mashambulio
ambayo hayakutarajiwa.
Ikumbukwe pia kuwa ni
CIA mpaka sasa ndio wanaoaminiwa kupanga njama na kumuua Rais Hugo Chaves wa
nchi hiyo.Rais Chaves alifariki kwa matatizo ya kansa jambo ambalo hata kabla
ya kifo chake alitoa angalizo kwa kusema Marekani inawaua viongozi kwa kutumia
teknolojia ya hali ya juu Hi-Tech
assasination ikiwemo kuwasababishia kansa ambayo aidha itawaua taratibu ama
haraka.Jambo hili linasahidiwa kwa kitendo cha aliekuwa mlinzi maalumu wa Rais
Chaves bwana Salazar kukimbilia Marekani na kupata hifadhi ya CIA mara tu baada
ya kifo cha Rais Hugo Chaves.
0 comments:
Post a Comment