Wasichana wengi
hujikuta wakipata ujauzito bila kupanga. Kwa hiyo hupatwa na mawazo ya kutoa
ujauzito huo bila ya kupima faida na hasara za kuutoa. Hata hivyo pamoja na
kuwa hairuhusiwi kisheria kutoa mimba (abortion) ambayo haina hatari kwa afya
ya mama, lakini ikilazimika, basi utoaji mimba ufanyike katika mazingira
salama, ambayo ni nadra kupatikana hasa katika mataifa machanga na ambayo
yanapiga marufuku utoaji mimba. Zifuatazo ni hatari zinazoweza kutokea wakati
na/au baada ya kutoa Mimba.
1. Kutokwa damu
nyingi, (Haemorrage) mfuko wa mimba una mirija mingi ya damu mahususi kwa ajili
ya kuhudumia kijacho kwa hewa na virutubisho. Utoaji mimba huweza kupelekea
kupasuka kwa mirija hiyo midogo kwa mikubwa kisha kuvuja na kusababisha
upungufu mkubwa wa damu wa ghafla (Shock) au hata kifo.
2. Kutoboka kwa
mfuko wa mimba (uterine wall perforation). Ikiwa utaalam hautakidhi au kwa
bahati mbaya, vifaa vitumikavyo katika utoaji vyaweza kutoboa mfuko wa mimba na
pia kuharibu ogani za karibu yake kama utumbo na kibofu cha mkojo.
3. Ugumba
(Infertility). Kutoboka kwa mfuko wa mimba au kuharibika kwa sehemu zingine za
uzazi kutokana na vifaa vya ovyo au utaalam usiokudhi kwaweza kusababisha
ugumba kwa muda au wa kudumu.
4. Kutungwa mimba
nje ya mfuko wa mimba (Ectopic Pregnancy).
5. Maambukizi ya
bacteria (Sepsis). Ikiwa usafi haukuzingatiwa, mchakato wa utoaji mimba huweza
kupelekea maambukizi na kisha homa kali.Piaikiwa kuna mabaki ya mimba
(products of conception) katika mji wa mimba,tatizo huwa kubwa zaidi na
kuhitaji huduma ya dharura ili kuepuka kifo.
Mambo ya
Kuzingatia.
- Hakikisha uduma, mtaalam na vifaa vinakidhi. Utahakikishaje?
- Hakikisha kuna usafiri wa haraka kwa ajili ya kupata rufaa kwa huduma zaidi endapo italazimika.
- Si salama sana kutoa ujauzito wa miezi zaidi ya 3,hasa katika mazingira ya uchochoroni. Katika ujauzito wa Miezi mitatu, mifupa huwa tayari imetengenezwa.
- Zingatia Sheria za Nchi juu ya suala la utoaji mimba.
Asante.
Dr. Chris Cyrilo
0 comments:
Post a Comment