Ugonjwa
wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose)
katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. Homoni aina
ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa
sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa
kuratibu sukari katika damu. Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na
kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa
cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la
mgandamizo wa damu (hypertension) au presha.
Asilimia
55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.
Mambo
haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha
upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).
1.
Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za
mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen
Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa
ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa
kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.
2.
Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya
mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo
(diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.
3.
Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa
kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo
yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.
Pia,
Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza
ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia
na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna
hiyo.
Tatizo
hili pamoja na mengine mengi yanayosababishwa na ugonjwa wa kisukari huweza
kuzuiwa au kupunguzwa kwa kuzingatia masharti ya kitabibu. Katika kliniki za
kisukari wagonjwa huelekezwa namna ya kudhibiti sukari ili isizidi kiasi cha
kuleta madhara makubwa kama haya.
Asante.
Dr.Chris Cyrilo.
0 comments:
Post a Comment