Leo
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo
amedhihirisha ukomavu wake wa kisiasa sio tu kwa kuitika wito wa jeshi la
polisi la kumtaka kwenda kuhojiana nae bali kwa kutoa rai kwa muheshimiwa Rais
Magufuli juu ya hatua ya serikali yake kutaka kuwaziba midomo wapinzani nchini.
Akihojiwa
kwa saa tatu na Kamanda wa Upelelezi mkoa wa kipolisi wa Temeke na Naibu Kamada
wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alisema Mambo kama haya ya kuwanyanyasa wapinzani yalikuwa
yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini sasa sote ni mashahidi
jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa na kwamba ni
muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia yao.
Jana
(Jumanne) jeshi la polisi lilizuia mikutano ya kisiasa mpaka hapo litakapotoa
tena taarifa ya kuruhusu mikutano hiyo hatua ambayo Zitto amesema sio sahihi kwa jeshi hilo kufanya namna
hiyo.Kiongozi huyo amenukuliwa akisema ni lazima kama chama cha ACT Wazalendo
waende mahakamani kupata tafsiri sahihi ya katazo hilo.
Juu ya kusiginwa
kwa demokrasia nchini kiongozi huyo alinukuliwa akisema “Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo
yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa
kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani
haina maana”.
“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu kwa
kunihoji tu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na
majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa
kutuhoji maswali,” amesema Zitto.
Zitto amemtaka Rais kuhakikisha serikali yake badala ya
kusigina demokrwasia inasaidia kuifanya ichanue na kuwa zama za kuongoza watu
kwa vitisho zimepitwa na wakati.
0 comments:
Post a Comment