Nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika Ya Mashariki wameamua kuimarisha chumi za nchi
zao kwa kuimarisha sekta za miundombinu na nishati.Katika bajeti zao
zilizowasilishwa jana, Kenya ambayo ndio inaongoza kwa uchumi mkubwa imepanga kutumia dola za kimarekani 22.8
bilioni wakati Tanzania imekadiria dola bilioni 13.5, Uganda dola bilioni 12
huku Rwanda ikikadiria dola bilioni 2.49 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Burundi
yenyewe haipo kwenye utaratibu huu wa kusoma bajeti kwa pamoja.
TANZANIA
Dr.Phillip Mpango |
Akiwakilisha
hotuba ya bajeti Waziri wa Uchumi na Mipango Phillip Mpango ameainisha kuwa
bajeti hii mpya itajikita katika kupambana na changamoto za mwananchi wa kipato
cha chini na kuweka misingi imara ya uchumi kwa ajili ya wale wa kipato cha
kati.Katika nchi ambayo deni la taifa ni dola za kimarekani bilioni 20.94 mpaka
kufikia Machi mwaka huu shunguli za maendeleo zimetengewa asilimia 40.
Pia
Tanzania imepanga kukopa shilingi trilioni 7.4 kutoka katika pato la ndani ili
kuziba mwanya katika mwaka huu wa fedha.Serikali pia itatumia shilingi trilioni
17.7 kama pesa za kuendeshea shuguli za kila siku na shilingi trilioni 11.8 kwa
ajili ya miradi ya maendeleo.Katika hilo zaidi ya shilingi trilioni 4.77 sawa
na asilimia 22.1 zimeelekezwa katika elimu.Waziri pia akatangaza ongezeko la
kodi kwa mvinyo na bia.Zaidi ya shilingi trilioni 18.4 sawa na asilimia 62.5 ya
bajeti imepangwa kupatikana kwa makusanyo ya ndani.
KENYA
Henry Rotich |
Kwa
upande wa kenya waziri wa fedha wa nchi hiyo Henry Rotich amesema katika bajeti
ya mwaka huu itajielekeza kwenye miundombinu na kilimo.Waziri akafuta kodi juu
ya chai na sukari.Sekta ya nishati ikapatiwa shilingi za kenya bilioni
39.9,reli ya kisasa ikatengewa shilingi za kenya bilioni 228.5 na barabara
shilingi za kenya bilioni 147.6
UGANDA
Matia Kasaija |
Uganda
yenyewe bajeti yake itajikita katika kuimarisha sekta ya nishati na miradi ya
miundombinu ya usafirishaji.Lakini pia itajikita katika sekta ya kilimo hasa
kukifanya cha kisasa na kuongeza mazao thamani ili yawezwe kuuzwa soko la
nje..Waziri wa fedha wa nchi hiyo Matia Kasaija alisoma hotuba hiyo yenye
makadirio ya shilingi ya uganda bilioni 26,361,alisema kuimarisha biashara ya
mafuta na gesi ndio itakuwa kipaumbele cha kwanza kwa mwaka wa fedha ulioanza
na hivyo serikali imetenga shilingi ya Uganda bilioni 188.2 katika kukamilisha
azma hiyo.
Hata
hivyo sehemu kubwa kabisa ya bejti ya mwaka huu ya Uganda imeelekezwa kwenye
wizara ya ajira kwa kutengewa shilingi ya Uganda trilioni 3.7 ikifuatiwa na
sekta ya elimu iliyopata shilingi ya Uganda trilioni 2.7 na sekta ya nishati
trilioni 2.4
Waziri
huyo pia aliongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi ya Uganda bilioni 343.46 mwaka jana mpaka bilioni 823.42 mwaka
huu ili kuongeza uzalishaji na biashara ya mazao ya kilimo.
0 comments:
Post a Comment