#10
Yahoo Stocks
Duniani sasa hivi wengi wanapenda kuwekeza kwenye
masoko ya hisa.Tofauti na miaka ya nyuma ambapo si wengi wa rika la ujana
walipendezwa na biashara hii sasa hivi hata vijana wanajihusisha na uwekezaji
wa aina hii.Basi apps hii imachukua nafasi kuliko unavyoweza kudhani.
#9
Apple Maps
Apple Maps inashika namba tisa.Ni application nzuri
sana inayokuonyesha dira na uelekezi popote duniani.
#8
Instagram
Labda hii watanzania wengi wangedhani ndio inayoongoza
maana ndio tumejikita huku lakini ukweli ni kuwa inashikilia namba nane.Watu
wanapenda kujipiga picha sana basi Instagram ndio penyewe katika kupost vitu
vya namna hiyo.
#7
Gmail
Hata hii si ngeni na sijui kama kuna mtu yupo kwenye
mtandao wa internet na hana account ya gmail itakuwa ni kioja.Shangaa inashika
namba saba.
#6
Google Maps
Yani ni waafrika tu ama watanzania ndio hatutumii sana
hii application lakini kwa nchi za wenzetu hii inatumika kuliko hata Instagram.Inashika
namba sita.
#5
Pandora Radio
Hapa Tanzania watu hawaijui ama kama wanaijua basi ni
wachache.Hii application unaweza kusikiliza muziki wowote bure.Ijaribu uone
utamu wake.
#4
Google Search
Hivi kuna mtu ana smart phone na hakuwahi kutafuta
chochote kwa kutumia google?.Hii aihitaji maelezo.Ipo namba 4.
#3
Google Play Store
Wo wo wo Hii haitaki nieleze sana yani ili upate apps
kirahisi sasa hivi ni lazima uingie hapa.Hii inashika namba tatu
#2
YouTube
Unataka kutazama video?kusikiliza muziki?kuangalia
clips mbalimbali za jambo lolote lile?Unaachaje kuifaham YouTube sasa?Ni apps
ya pili duniani kwa kutembelewa na mafanikio.
#1
Facebook
Sidhani kama utashangaa kusikia kuwa facebook ndio
inashikilia namba moja kwa kutembelewa na watu wengi duniani.Hakika ina haki
hiyo.Hii ndio kiboko yao.
0 comments:
Post a Comment