Israeli ilijitangazia uhuru wake Mei 14, 1948 kufuatia uhuru huo mataifa
ya kiarabu Misri, Lebanon, Syria, Jordan na Iraq yaliivamia Israeli na kuzuka
vita baina yao. Israeli iliibuka kidedea ikiyateka maeneo zaidi ya ramani ya
awali na kugawa mji wa Yerusalem. Mwaka 1964 wapalestina walianzisha chama cha
Palestinian Liberation Organization (PLO) ambacho hakikutambuliwa na Israeli.
Katika vita vya Siku Sita 1967 vya Israeli na waarabu ambavyo Israeli ilishinda
kwa kishindo ikiacha hasara kubwa kwa maadui zake viliifanya nchi hiyo
kujiongezea ukubwa mara tatu ya ule wa awali.
Siri ya ushindi wa vita hivyo ulitokana na mbinu na maandalizi mazuri
yaliyokuwa yamefanywa na hasa ni kule kuvamia kabla ya adui hajakushambulia.
Kama wangesubiri washambuliwe basi Israeli ingefutwa katika ramani ya dunia
kama waarabu walivyokuwa wameazimia.
Ariel Sharon.Kiongozi wa Israel na aliekuwa mkuu wa majeshi mwaka 1948 |
Vita hiyo ya 1967 Israeli ilipigana na Misri, Syria, Lebanon, Jordan
zikisaidiwa kijeshi na Sudani, Iraq, Algeria nchi zilizopeleka askari na
silaha, Urusi ikisaidia mataifa hayo kwa wingi wa silaha. Kabla ya vita mataifa
ya Marekani, Uingereza na Ufaransa yalipeleka silaha kwa Israeli na kuifanya
isiwe na wasiwasi katika matumizi ya silaha. Nini chanzo cha vita hiyo? Israeli
na majirani zake walikuwa wakiishi katika hali ya uhasama tangu 1948 baada ya
azimio la umoja wa mataifa la mwaka1947, lililoamuru kugawanywa kwa nchi hiyo,
waarabu walikuwa bado wanayo hasira juu ya uwepo wa taifa hilo mashariki ya
kati. Viongozi mbalimbali wa nchi za kiarabu waliazimia kuifuta Israeli kwenye
ramani ya dunia. Israeli iligombana na Syria ilipoanza mradi wa ujenzi wa
miundombinu ya maji kuyatoa mto Jordan na kusambaza katika nchi hiyo. Jeshi la
Syria likatumia milima/miinuko ya Golan ilinayopata futi 3000 juu ya Galilaya
kushambulia vijiji na mashamba.
Gamal Abdel Nasser |
Mashambulio ya Syria yaliongezeka sana mwaka 1965 -66, Israeli
ikilalamika Umoja wa Mataifa ambao ulisisitiza kuacha mapigano bila kuchukua
hatua yoyote kwa Syria ambapo hata ulipotoa azimio la kulaani mashambulizi hayo
yalipingwa kwa kura ya veto na Urusi. Mashambulizi hayo yalienda sanjali na
vitendo vya hujuma kali na ugaidi dhidi ya taifa hilo ambapo mwaka 1965 Rais wa
Misri Gamal Abdel Nasser alisema “hatutaingia Palestina nchi ikiwa imefunikwa
kwa mchanga bali damu”. Baada ya miezi michache Nasser alisema tena kuwa azma
ya waarabu ni kuona wapalestina wanakombolewa, kwa kifupi ni kuiondoa dola ya
kiyahudi kwa maangamizi. Aprili 7, 1967 Syria ikitumia ndege aina ya MiG21
ilizokuwa imepewa na Urusi ilishambulia kijiji cha Kibbutzim kutokea Miinuko ya
Golan, Jeshi la Israeli lilitungua ndege sita za Syria.Urusi iliipa taarifa
isiyo sahihi Syria kuwa Israeli inajiandaa kwa vita licha ya Israel kukanusha
lakini Syria ilijipanga ikiweka makubaliano ya ushirikiano na Misri.
Yeser Arafat.Aliyepata kuwa kiongozi wa Palestina |
Tarehe 15 Mei, 1967 siku ya uhuru wa Israeli, majeshi ya Misri yalivuka
kuelekea Sinai karibu na mpaka na Israeli ambapo siku tatu baadaye tarehe 18
jeshi la Syria likajipanga kwa vita katika milima ya Golan. Baada ya majeshi ya
Misri na Syria kujipanga kwa vita, Gamal Abdel Nasser aliamuru jeshi la umoja
wa mataifa UN Emergency Force (UNEF), lililokuwa Sinai likiikinga Israeli tangu
1956 kuondoka mara moja bila kushirikisha umoja huo. Mei 22, Misri ilifunga
mlango bahari wa Tiran na kuzuia meli zote za kutoka mashariki kuingia Israeli
na kuzuia meli za Iran zilizokuwa zinapeleka mafuta ya petroli na kuifanya nchi
hiyo kutokuwa na njia inayopitika (uamuzi wa Misri ulikiuka sheria za
kimataifa). Radio Sauti ya Waarabu ikisema “kwa kuwa sasa jeshi la kimataifa
lililokuwa linaikinga Israeli limeondoka hatutavumilia zaidi wala kulalamika
umoja wa mataifa ila jambo moja tutakalofanya ni kuipiga vita na kutokomeza
siasa za kizayuni”.
Hafez Assad |
Naye waziri wa ulinzi wa Syria Hafez Assad alisema “majeshi yetu yako
tayari kuifuta Israeli” nakuu kwa kimombo ‘Our forces are now entirely ready
not only to repulse the aggression, but to initiate the act of liberation
itself, and to explode the Zionist presence in the Arab homeland. The Syrian
army, with its finger on the trigger, is united….I, as a military man, believe
that the time has come to enter into a battle of annihilation” alisema hayo Mei
20, 1967. Rais wa Marekani Johnson alilaani na kusema kitendo cha Misri ni
kinyume na sheria ya bahari iliyopitiwa mwaka 1958 ambapo umoja wa mataifa
ulitambua haki ya Israeli kutumia mlango bahari wa Tiran (Straits of Tiran)
kupitisha meli.
Nasser aliendelea na vitisho akiitaka Israeli kuingia vitani akidai kuwa
hawatasikiliza shauri lolote la masikilizano kwani wao wako vitani na Israeli
tangu mwaka 1948. Aliongeza kusema kuwa majeshi ya Misri, Jordan, Syria na
Lebanon yametulia mipakani mwa Israeli na nyuma yao yapo majeshi ya Irak,
Algeria, Kuwait, Sudan, Saudi Arabia na ulimwengu wote wa kiarabu. Alijigamba
zaidi kwa kusema kwa tendo hili dunia yote itastaajabia na kujua kuwa waarabu
wapo wamejizatiti kwa vita. Rais wa Iraq Abdur Rahman Aref alisema “Uwepo wa
taifa la Israeli ni kosa ambalo ni lazima lirekebishwe, huu ni wakati wa kufuta
aibu ambayo tumekuwa nayo tangu 1948, lengo letu ni kuifuta Israeli kwenye
ramani”. Irak ilipeleka majeshi yake Juni 4 kujiunga na Misri, Jordan na
Syria.Majeshi ya kiarabu yanayokadiliwa askari 465,000, zaidi ya vifaru 2,800,
na ndege 800 viliizunguka Israeli.
Rais Johson wa Marekani |
Kipindi hicho Israeli ilikuwa kwenye hali ya tahadhari kwa wiki tatu
muda huo iliutumia kuingiza silaha toka mataifa ya magharibi Marekani, Ufaransa
na Uingereza. Silaha zilishushwa katika mji wenye bandari wa Haifa. Israeli kwa
kuwafahamu adui zake walivyo waliwafanyia kamchezo ka hadaa, kwanza ilifungua
mpaka wake na Misri ili kuruhusu wapelelezi wa Misri kuingia na kutoka. Pili
oparesheni ya kuhamisha silaha zilizowasili katika mji wa Haifa wakazipeleka
ghuba ya Aqaba eneo lenye pori na miamba wakati wa mchana na kuzirudisha Haifa
usiku na kuzihifadhi kwenye mahandaki.
Jambo jingine lililowasaidia Israeli ni hadaa iliyofanywa, Waarabu
walipotangaza vita na kuitisha Israeli, iliwaita makamanda wote waliokuwa
likizo kurudi kazini na mawaziri waliokuwa ziarani kurudi mara moja, jambo
lililofanywa na Misri pia. Baada ya wiki hizo tatu za maandalizi ya nguvu
Israeli ikatangaza kuwa makamanda waliokuwa likizo waendelee na likizo zao
inaonesha waarabu walikuwa wanawatisha tu hakutakuwa na vita. Kipindi hicho Marekani ilijaribu kuzuia vita kwa kuishauri Misri
kusitisha mpango wa vita lakini haikuwezekana kumshauri raisi wa Misri Gamal
Abde Nasser hali iliyomfanya Rais wa Marekani Johnson kuonya kuwa “Israeli
haitakuwa pekee vitani labda ikitaka kuwa hivyo”.
Levi Eshkol
|
Juni 5, 1967 waziri mkuu wa Israeli Levi Eshkol aliamuru kuishambulia Misri, hapo Israeli ilikuwa peke yake, lakini yenye makamanda waliojizatiti kwa mkakati maalum. Jeshi lote la anga la Israeli ukiacha ndege 12 tu ziliachwa kulinda anga la Israeli, majira ya saa 1.14 asubuhi (saa moja asubuhi) walipiga mabomu viwanja vyote vya ndege za kivita vya Misri wakati marubani wa ndege hizo wakipata kifungua kinywa. Ndani ya masaa mawili ndege 300 za Misri zilikuwa zimeshapigwa mabomu na kuharibiwa kabisa, masaa machache baadaye ndege za Israeli zilishambulia majeshi ya anga ya Jordan na Syria na kiwanja kimoja cha Irak. Jioni ya siku ya kwanza ya vita ndege zote za Misri na Jordan na nusu ya ndege za Syria zilikuwa zimeharibiwa zikiwa viwanjani, (ujanja wa kuzipiga kabla hazijaruka ulitumika).
Juni 5, 1967 waziri mkuu wa Israeli Levi Eshkol aliamuru kuishambulia Misri, hapo Israeli ilikuwa peke yake, lakini yenye makamanda waliojizatiti kwa mkakati maalum. Jeshi lote la anga la Israeli ukiacha ndege 12 tu ziliachwa kulinda anga la Israeli, majira ya saa 1.14 asubuhi (saa moja asubuhi) walipiga mabomu viwanja vyote vya ndege za kivita vya Misri wakati marubani wa ndege hizo wakipata kifungua kinywa. Ndani ya masaa mawili ndege 300 za Misri zilikuwa zimeshapigwa mabomu na kuharibiwa kabisa, masaa machache baadaye ndege za Israeli zilishambulia majeshi ya anga ya Jordan na Syria na kiwanja kimoja cha Irak. Jioni ya siku ya kwanza ya vita ndege zote za Misri na Jordan na nusu ya ndege za Syria zilikuwa zimeharibiwa zikiwa viwanjani, (ujanja wa kuzipiga kabla hazijaruka ulitumika).
Misri iliyokuwa na nguvu za kijeshi na jeshi kubwa la ardhini lenye
vifaru na magari ya vita ilianza matayarisho ya kuyavusha kwenye mfereji wa
Suez (madarajani) likafaulu kuvusha askari 20,000 hadi penisula ya Sinai.
Israel ikiwa inaangalia mwenendo wote wa majeshi ya Misri iliacha operesheni
hiyo ifanyike ya uvushaji askari na silaha kuelekea Sinai na kisha ikatuma
ndege zake kuvunja madaraja ya Suez na kuhakikisha hakuna msaada wa kijeshi
wala chakula utakaovuka kusaidia kikosi kilichokwisha vuka. Kisha vilianza vita
vya ardhini ambapo mapigano makubwa ya kihistoria ya vifaru yalitokea baina ya
majeshi ya Misri na Israeli katika jangwa la Sinai. Baada ya Jordan kushambuliwa
wapalestina wapatao 325,000 walioishi Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan
walilazimika kukimbia na kwenda nchini Jordan kuepuka vita.
Kikosi kidogo cha mashujaa wa Israeli kiliwekwa kuzuia majeshi ya Syria
wakati vita vikali vikiendelea baina ya Israeli na Misri na Jordan hadi
walipoona wamedhoofisha majeshi hayo ndipo kikosi kizima cha jeshi la anga
kiliposhambulia ngome ya Syria kwenye milima Golan, Juni 9, baada ya siku mbili
za mashumbulizi ya nguvu walifaulu kupenya safu ya Syria. Baada ya siku sita za
mapigano Israeli ilikuwa na uwezo wa kuingia Cairo, Damascus na Amman bila
kikwazo, wakati huo lengo la kuiteka Sinai na Miinuko ya Golan lilikuwa
limefikiwa. Viongozi wa Israeli hawakuwa na nia ya kupiga miji mikuu ya nchi
hizo, jambo ambalo walikuwa na uwezo nalo.
Dean Rusk |
Zaidi ya hayo Urusi ikiwa imechanganyikiwa na mafanikio ya Israeli ikawa
inatishia kuingilia vita. Wakati huo waziri wa Mambo ya nje (Secretary of
State) wa Marekani Dean Rusk aliishauri Israeli kukubali wito wa kusimamisha
mapigano, Israeli ilikubali Juni 10 ilisimamisha mapigano. Ushindi wa Israeli
uliigharimu. Katika kushambulia milima ya Golan wanajeshi 115 wa Israeli
walipoteza maisha ikipoteza ndege 46 kati ya 200 wakati upande wa waarabu Misri
askari 15,000, Syria 2500 na Jordan 800. Mwisho wa vita Israeli ilikuwa
imejiongezea ukubwa wa eneo mara tatu kutoka maili za mraba 8000 hadi 26,000,
ushindi huo uliifanya Israeli kuutwaa mji wa Yerusalem, mkono bahari wa Sinai,
Golan, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Licha ya vita hiyo Israeli iliwashauri wapalestina kuendelea kuishi
chini ya utawala wa Israeli ambapo baadhi ya familia za wapalestina zilizokuwa
zimetengana waliweza kuungana na wengine hawakuwa na imani na Israeli. Mwezi
Novemba 1967, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio na 242
lililowataka Israeli na Waarabu kuwa na amani ambapo Israeli ilitakiwa kuondoka
katika Ardhi ilizoteka kwa makubaliano ya kuwa na amani na majirani zake.
Mwandishi maarufu wa habari za Waarabu katika Israeli Don Peretz aliyetembelea
Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan siku chache baada ya vita alithibitisha kuona
jinsi Israeli ilivyojitahidi kurejesha hali ya kawaida ya maisha na kuzuia
kuhama kwa waarabu maeneo hayo.
Golder Meir |
Mgogoro mwingine uliibuka mwaka 1973, vita vilivyojulikana kwa jina la
Yom Kippur, waziri mkuu wa Israeli akiwa Golder Meir (Iron Woman) ambavyo
Israeli ilipigana bila ya maandalizi yoyote kwani ilishambuliwa kwa kustukizwa.
Golder Meir ambaye alichaguliwa kuchukua nafasi ya Levi Eshkol kufuatia kifo
chake cha ghafla Februari 26, 1969 na Meir kuanza kazi hiyo Machi 17 mwaka huo
akiwa na sifa kem kem ikiwepo ya kufanikisha serikali ya mseto mwaka 1967 baada
ya vita ya siku sita chama cha Mapai kilijiunga na vyama vingine vya Rafi na
Ahdut Havoda na kuunda Israel Labour Party.
Ni katika kipindi cha Golder Meir kabla ya vita ya Yom Kippur yalitokea
mauaji ya wanamichezo wa Israeli huko Ujerumani waliposhiriki michezo ya
Olimpiki 1972 mauaji yaliyojulikana kama Mauaji ya Munich ambapo jumla ya
wanamichezo 11 waliuawa na kikundi cha wapalestina kiliichoitwa Black September
Organization. Kwa ujasiri mkubwa baada ya kuona jumuia ya kimataifa haijachukua
hatua stahili, Golder Meir aliamuru shirika lake la kijasusi Mossad kuwasaka na
kuwaua wote walioshiriki kupanga mauaji hayo ambayo watekaji nyara walidai
kuachiwa huru kwa wafungwa 363 wa kipalestina na wengine walioshikiliwa katika
magereza ya Israeli. Mpango huo ulijulikana kama Operesheni Ghadhabu ya Mungu
au Operesheni Singe. Katika kiwango cha juu cha ufanisi, Mossad iliwachukua
siku 60 tu kuangamiza kikundi chote cha kigaidi ambacho kilikuwa kimesambaa
Syria, Jordan na Palestina, yalikuwa ni mauaji ya siri chini ya Kidon ya
Mossad.
Katika operesheni hiyo ambayo ililenga kulipiza kisasi kwa wote
waliohusika kupanga mauaji hayo wakiwepo baadhi ya wanachama wa kundi la PLO na
Black September Organization ambapo mauaji yalitekelezwa kwa siri na kundi la
watu 15 waliogawanywa katika makundi matano.
Vita ya Yom Kippur au Ramadhan war au vita vya Oktoba kama
vinavyojulikana vilipiganwa tangu Oktoba 6 hadi 26 mwaka 1973 umoja wa mataifa
ulipoilazimisha Israeli kusimamisha vita na hasa baada ya Israeli kukizingira
kikosi kikubwa cha tatu cha Misri (Third Army). Mwanzoni waarabu walionekana
kushinda vita na kusababisha hasara kubwa kwa jeshi la Israeli lakini upepo
uligeuka ambapo Israeli iliwapiga adui zake na kupenya hadi ukingo wa magharibi
wa bahari ya Shamu (walivuka mfereji wa Suez) Hata hivyo Idara ya Usalama ya
Israeli ililaumiwa kwa kutokuwa makini kwani walionywa mara kadhaa kuhusu
kusudio la waarabu la kuishambulia Israeli.
Mohamadou Abbas.Aliyepata kuwa Kiongozi wa Palestina |
Vilianza kwa mashambulizi ya ghafla ya Misri na Syria siku ya sikukuu
kubwa ya wayahudi ya kidini ambapo mataifa hayo mawili yaliishambulia Israeli
kwa nguvu na kuonekana kama watashinda vita katika saa 24 hadi 48 ya kwanza
baada ya hapo hali iligeuka. Katika wiki ya pili ya mapigano Syria ilikuwa
imesukumwa kutoka milima ya Golan na kwa upande wa Misri vikosi vilisukumwa
hadi kusini mwa Sinai na kisha kikosi cha Israeli kikapenya kati ya vikosi viwili
vya Misri na kuvuka mfereji wa Suez na kukizingira kikosi cha tatu (Third Army)
cha Misri. Jeshi la Misri lililokuwa limevuka mfereji wa Suez (mpaka wa vita
vya 1967, mstari wa kusimamisha mapigano) likajigawa Ukanda wa Gaza na kusini
ukingo wa mashariki wa Suez likavunja ngome iliyojengwa iliyoigharimu Israeli
dola 500 za kimarekani ambayo ilipewa jina la Bar Lev Line kwa heshima ya
Jenerali Chaim Bar-Lev.
Kuzingirwa kwa kikosi huko kuliipa nguvu Israeli wakati wa mazungumzo
yaliyokuwa kiini cha mkataba wa Camp David, Israeli ilitaka kukiangamiza kikosi
hicho ambapo Misri ilibidi ijisalimishe ili kuokoa maisha ya wanajeshi wapatao
20,000. Marekani ilitumia mwanya huo kuilazimisha Misri kufuta maombi ya msaada
iliyokuwa imeomba toka Urusi na kuahidi kuisaidia na hivyo kupunguza ushawishi
wa Urusi eneo hilo ambapo mambo yalihitimishwa kwa mkataba wa Camp David
uliopatanisha Israeli na Misri hadi leo. Baada ya kifo cha Gamar Abdel Nasser
rais wa Misri alitawala Anwaar Sadat ambaye alikuwa ametangaza mwaka 1972 kuwa
ameamua kuingia vitani na Israeli na kwamba ameandaa wanajeshi milioni moja
ambao wako tayari kujitoa muhanga ili kukomboa maeneo ya Sinai.
Kwa kauli hiyo mwishoni wa 1972 alinunua ndege za kivita MiG-21,
makombora ya kutungulia ndege ya SA-2, SA-3, SA-6 na SA-7 , na vifaru aina ya
T-55 na T-62, silaha za kulipulia vifaru RPG-7 na makombola ya vifaru ya AT-3
kutoka Urusi. Sadat akiipa jina la Operesheni Badr (neno la kiarabu lenye maana
ya mwezi mpevu) akilinganisha na Vita vya Badr ambavyo waislam waliwashinda
Wakuraish wa Maka akikusudia kurudisha heshima ya Waarabu waliyopoteza katika
vita ya 1967. Habari za kijasusi ziliifikia Israeli kuwa Misri ilipanga
kuivamia Israeli lakini isingefanya vile bila kupokea ndege za MiG-23 na
makombola ya Scud ambayo yangetumika kuibomoa miji ya Israeli.
Yuri Androve |
Taarifa hiyo iliifanya Israeli isiwe makini na kudhani vita isengetokea
katika muda mfupi hivyo. Mikakati ya vita iliyofanywa na Sadat na mwenzie Assad
wa Syria ilikuwa kuivamia Israeli siku ya sikukuu kubwa ya Yom Kippur ambapo
ilikuwa ni siku ya mapumziko, hakuna kuwasha mioto wala kuendesha magari na
hivyo kufanya kila kitu kuwa kimya kabisa. Hali hiyo iliwasaidia Israeli kwani
walipovamiwa ghafla iliwawia rahisi kutumia barabara kujipanga haraka kwani
hakukuwa na msongamano wa magari barabarani, pia iliwakusanya maaskari wa akiba
kirahisi kwani wengi walikuwa kwenye masinagogi wakisali. Mbinu nyingine
iliyotumiwa na Misri ni kuwapa likizo askari wa akiba ambapo Nasser aliruhusu
askari 20000 kwenda mapumzikoni na wengine kwenda Hija.
Usiku wa Septemba 25 mfalme Hussein wa Jordan aliruka kwa ndege kwa siri
hadi Tel Aviv kumwonya waziri mkuu wa Israeli Golder Meir juu ya shambulio
lililopangwa dhidi yake jambo ambalo walipuuza. Mwezi huo Israeli ilipata
maonyo kumi na moja toka vyanzo vya kuaminika lakini mkuu wa Mossad Zvi Zamir
alipuuza. Lakini Golder Meir, Moshe Dayan, na Jenerali David Elazar walikutana
saa 2:05 asubuhi ya siku ya Yom Kippur, masaa sita kabla ya shambulio. Golder
Meir alikataa kuanzisha shambulio akihofia kutopata msaada wowote toka nje.
Wakati huo nchi za Ulaya zilikuwa zimeacha kuisaidia Israeli silaha. Mara
waziri huyo alipotoa uamuzi alipokea ujumbe kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Henry Kissinger kuwa Israeli isishambulie isubiri tu. Vita hiyo ambayo
kwa sehemu kubwa Israeli ililemewa na kupata hasara kubwa kwani katika masaa 27
ya kwanza ilikuwa imepoteza ndege 30 na vifaru 300 katika shambulio la Misri la
Bar-Lev huku jeshi hilo la Misri likiwa limesonga mbele kwenye jangwa la Sinai
kilomita tano.
Israeli ilibidi ibadili mbinu za kivita kwani makombora ya ulinzi wa
anga ya SAM yaliwazidi nguvu, wakaamua kutumia jeshi la miguu (Infantry),
kikosi hicho kilifaulu kwa sehemu kubwa hadi kupenya hadi kwenye safu
yalikowekwa makombora hayo na kuyaharibu na hivyo kudhoofisha mfumo wa
kujikinga wa Misri. Baada ya kudhoofisha mfumo huo wa ulinzi ndipo jeshi la
anga la Israeli likazidisha mashambulizi.
Benjamin Netanyahu.Waziri Mkuu wa sasa wa Israel |
Siku iliyofuata, Oktoba 15, Israeli ilianzisha Operesheni Abiray-Lev
(operesheni ya mashujaa). Divisheni iliyoongozwa na Meja Jenerali Ariel Sharon
ilishambulia safu za jeshi la Misri eneo la Ismailiya kati ya kikosi cha pili
kilichokuwa kaskazini na cha tatu kusini ( na kufaulu kupenya hadi Suez na
kuvuka. Baada ya siku chache Israeli ilijenga madaraja manne kuvuka mfereji wa
Suez mwisho wa vita Israeli ilikuwa ndani ya Misri kilomita 101 kutoka mji wa
Cairo. Kwa upande wa Syria hali ilikuwa tofauti kidogo, pamoja na kuwa na
silaha kama zile za Misri vita vilikuwa vikali ambapo ndege za Israeli zikikwepa
kutunguliwa zilikuwa zikipita uwanda wa chini wa Jordan kisha kuibukia Syria na
vifaru vingi vilipelekwa huko. Viongozi wa Israeli waliithamini sana milima ya
Golan na hivyo kupeleka nguvu zote hapo kwani jeshi la Syria lingefaulu kuteka
milima hiyo ingelikuwa rahisi kupita hadi Tiberias, Safed, Haifa, Netanya, na
Tel Aviv.
Askari wote wa akiba walipelekwa milima ya Golan wakipewa vifaru na
kuendelea na mapambano, hapo ndipo alipoibuka shujaa wa vita hivyo Luten Zvika
Greengold ambaye alifika jioni hiyo kwenye uwanja wa mapambano, alikuwa peke
yake akitumia kifaru chake kupambana na majeshi ya Syria akiyapiga hadi msaada
ulipofika. Saa 20 baadaye Zvika Force jina alilobatizwa alitumia kifaru chake
kuingia katikati ya vifaru vya Syria na kuvipiga huko na huko ambapo alibadili
vifaru sita, wakati mwingine akijichanganya na kikosi cha vifaru mara nyingine
peke yake, alijeruhiwa, aliunguzwa moto lakini aliendelea na mapambano kwa
kitendo hicho Zvika alitangazwa kuwa shujaa wa vita hivyo. Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio namba 338 la kusitisha vita baada ya
Marekani na Urusi kukubaliana Oktoba 22 ambalo lilianza kutekelezwa saa 12
baadaye.
Baada ya kuanza utekelezaji wa azimio hilo Misri ilishambulia mara
kadhaa vikosi vya Israeli ikiharibu vifaru 9, kwa kulipiza kisasi Israeli
ilielekeza majeshi yake kusini na kukizingira kikosi cha tatu cha Misri baada
ya Jenerali David Elazar kuomba idhini toka kwa Moshe Dayan kwani zoezi la
kusimamisha mapigano lilianza kutekelezwa wakati Israeli imebakiza mita chache
kufikia malengo wakateka barabara kuu ya Cairo kwenda Suez. Asubuhi ya Oktoba
23, Urusi iliilaumu Israeli kwamba majeshi yake yalionekana yakielekea kusini
Henry Kissinger akampigia simu Golder Meir kuwa unawezaje kutambua mstari wa kusimamisha
mapigano jangwani ambapo Meir alimjibu kuwa wote watajua tu akiwa na maana
watajijua na jeuri yao, muda mfupi baadaye Kissinger alipata taarifa za
kuzingirwa kwa kikosi cha tatu (Third Army).
Henry Kissinger alivyo kwa sasa |
Kissinger aligundua kuwa hiyo ni nafasi ya pekee kwa Marekani kuibana Misri ili
kuiondoa kwenye ushawishi wa Urusi, kwa kweli Misri haikua na ujanja wowote
zaidi ya kuitegemea Marekani kuizuia Israeli isikiangamize kikosi
kilichozingirwa ambacho hakikuwa na chakula wala maji. Wakati huo Rais wa Urusi
Leonard Brezhnev alimtumia barua Rais wa Marekani Richard Nixon akisema kuwa
Urusi na Marekani kwa pamoja visimamie usitishaji huo wa mapigano vinginevyo
Urusi ingeingilia kuisaidia Misri. Urusi ilikuwa imeshaandaa vikosi na baadhi
yake ikawa imevisafirisha toka Urusi hadi kwenye kituo chake cha kijeshi cha
Yugoslavia na kupeleka kikosi cha wanamaji 40,000 kwenye bahari ya
Mediterrenea. Kwa bahati mbaya barua hiyo ilifika Nixon akiwa amelala hivyo
Kissinger na maafisa wengine wa Ikulu akiwemo Katibu wa ulinzi James
Schlesinger, Mkurugenzi wa CIA William Colby na Mkuu wa White House Alexander
Haig (Kashfa ya Watergate ikiwa kileleni) waliishughulikia.
Wakubwa hao bila kumshirikisha Rais Nixon wakajibu kwa jina la Nixon kwa
Urusi na kuiambia Misri ijitoe katika ushawishi wa Urusi vinginevyo Urusi
ikiingilia na wao wataingia vitani, hilo likawa tishio la vita ya tatu ambayo
ingekuwa ya Nuclear. Urusi ilishangaa na hofu iliyowakumba Marekani hata mkuu
wa KGB Yuri Andropov akasema hali ni tete hatuwezi kuruhusu vita ya tatu.
Asubuhi yake Misri ilikubali ushauri wa Marekani na kutangaza kufuta ombi la
msaada iliyokuwa imeomba awali na Urusi ikakiri kushindwa vita kwa waarabu na
huo ukawa ndiyo mwisho wa mgogoro. Kutekelezwa kwa wito wa kusimamisha mapigano
baina ya Misri na Israeli kuliichanganya Syria iliyokuwa imejiandaa upya
kuishambulia Israeli tarehe 23 Oktoba baada ya kutafakari ikajua kuwa nguvu
yote ya Israeli ingehamia kwake na kupiga Damascus hivyo Assad akatangaza
kusimamisha mapigano Oktoba 23, na Irak ikawarudisha nyumbani askari wake. Hata
hivyo baada ya vita hiyo Golder Meir alijiuzulu kufuatiwa lawama za kutojiandaa
kwa taifa hilo kivita (utayari wa vita) baada ya tume ya Agranat Commission
kuelekeza lawama zote kwake na Yitzhak Rabin akamrithi mnamo Juni 3, 1973.
Mwaka 1975, Meir alituzwa Tuzo ya Israeli ( Israel Prize ) kwa mchango wake
maalum kwa taifa la Israel. Alifariki Disemba 8, 1978 kwa saratani mjini
Jerusalem akiwa na umri wa miaka 80.
Atakaye ubariki uzao wa Israel naye atabarikiwa, atakayeulaani uzao wa
Israel naye atalaaniwa daima
Makala hii ipo katika kitabu kiitwacho
"Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi" kilichoandikwa na Yericko Nyerere.
0 comments:
Post a Comment